Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tunazuga kama siyo ishu ila ndani tunaumia sana. Ubingwa ulikuwa nje nje tunaouna ingawa kiuhalisia hatukutegemea kukimbiza vile. Nahisi tulikuwa Bado tunashangaa Ile situation tukaamua turudie maisha tuliyoyazoea.
Kiwewe cha kuongoza ligi
Hangover za kuwa kileleni



Uzuri wako Mkuu huwa unasema ukweli.
 
😁😁 Nakubali mkuu.

Me enzi zangu washkaji walikuwa wananiita Dembele, nilikuwa nikishika mpira napita mbele ya msitu na sipotezi, ilikuwa combination ya minguvu na "udambwidambwi" hiyo mishuti sasa 😁 kipa utaomba poo. Sema ndo hivyo wazazi hawasapoti vipaji
 
Vipaji vingi vinapotea mtaani, kwetu shule ndio ilikuwa kipaumbele, ila ningeweka umakini kwenye game huenda mingekuwa mbali sana.
Kuna kipindi nilikuwa sina mazoezi, shule yetubhaikuwa na mambo ya michezo, ilivyotokea yale mashindano ya shule za sekondari tukapangwa, mwalimj wetu alikuwa ni mkenya anaioenda saana arsenal, mara kibao kanifumania nimetoroka shule niko mtaani nacheki game, siku ya kwanza kunifuma ilikuwa msala lakini kwa kuwa mshabiki wa arsenal na class nilikuwa fresh haikuwa kesi kubwa sana.
Sasa yule ticha alitupambania kwa mkuu wa shule tukacheze ile game, aana wale masister(wahindi) walikuwa wameshatia ngumu, kweli tukapiga mazoezi siku 3, siku ya 4 game..
Mie nilichelewa kufika, nikakuta game ishaanza, nikaingia kipindi cha pili.
Aisee nilicheza kama namba 10, timu ilikuwa imekufa pale, aisee nilichowafanya ile timu pinzani kwa dk 15, 20 hivi kabla pumzi kisoda hazijakata ni balaa uwanja ulikuwa kila nikipatabmpira unatapika, uwanja ulikuwa wa wapinzani wetu lakini nilioata mashabiki kinooma, game inaisha watu wananisherehekea japo tulipigwa 4-2, mademu, washikaji wa shule ile wanakuja kunipa pongezi.
Kauli moja naikumbuka vizuri saan, alikuja beki wao, ambae si chini ya mara 3 nilimlambisha mchanga akaniambia "mwanangu we ni fundi saana, inaonekana huna mazoezi ila unaujua saana mpira, ungezaliwa ulaya ungecheza timu kubwa bila shaka"
Nikaondoka nimepata hela za wanakijiji.

Aisee hili tukio sintosahau, ika ndio hivyo tena, sasa hivi miguu yetu tunagombania daladala za mbagala.
 
🤣🤣🤣...hapo mwishoni umeua mkuu
 
Wazazi wetu mpira walikuwa wanaona uhuni
 
Wazazi wetu mpira walikuwa wanaona uhuni
Kabisa, waliona shule ndio sehemu ya kutobolea tu. Wale niliocheza nao na kukubali viwango vyao wachache wamecheza premier league, kuna wa2 hivi hawa bahati sio yao na wanajua haswaa na wameupambania saana mpira, kifupi wanaudai mpira, ila bahati sio yao kabisa, wamecheza mpaka ligi daraja la kwanza, hawajabahatika kupiga premier na umri ndio ushaenda.
Kuna wawili hawa wanajua mpira waliupmbania lakini wamefelishwa na vitu fulani, huyu mmoja ni jamii ya kina baloteli, haruna moshi, bangi mtu uwanjani huwa anatusikiliZa wachache mnoo.
Huyu mwingine ni kipa shida huyu mjanja mjanja hachelewi kuuza mechi, yaani ye kwenye pesa hana dhamana. Hiki kimemuangusha sana.
 


Arsenal wako tayari kumuunga mkono Mikel Arteta kwenye dirisha la usajili la Januari, vyanzo vimeiambia Football Insider. Inaaminika wakuu wa klabu wako tayari kutumia hadi £50m kununua mchezaji mmoja, huku safu ya kiungo ikipewa kipaumbele.

[@footyinsider247]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…