Wakuu wenzangu mambo vipi inakuwaje?
Mzee Wenger ile Jumapili jioni alikaa kikao cha dharura pamoja na kamati yake yote ya ufundi inayojumuisha maskauti wote na makocha wengine wasaidizi.
Wenger akasema pesa itolewe na wale wachezaji wote ambao Arsenal imekuwa ikiwaulizia wauliziwe tena kufikia leo. Wakti huo huo Park Chu-Young alikuwa yupo London akifanyiwa uchunguzi wa Afya yake na matokeo yakawa ok na akaweka saini mkataba wa miaka minne. Kwa vile ana miaka 26 akifikisha miaka 30 atakuwa anaongeza mwaka au miaka miwili.
Park Chu-Young
Hii pia itakuwa ikifuata mpango mpya wa usajili (Transfer Policy Strategy) wa miaka mitano ambao Wenger amekwishapanga na CEO Ivan Gazidis.
Baada ya hapo Santos beki wa kushoto wa timu ya taifa Brazil nae atasaini mkataba na Arsenal FC unaogharimu paundi milioni 6.2. Santos ana miaka 28 na amechezea timu za Corinthias na Fenerbahce.
Andre Santos.
Kwa kuwa Club ya Bolton Wonderers wanaringa na kudai milioni 17 kwa Gary Cahil basi Arsenal ikabidi wawasiliane na kocha wa wa timu ya taifa ya Ujerumani Mr Joachim ambayo inajiandaa kucheza na Austria, kumwomba amruhusu Per Mertesacker aje London asubuhi hii na inasemekana amesaini mkataba tayari ila ilikuwa amalizie medical.
Per Mertesacker beki imara wa Werder Bremen na timu ya taifa ya Germany.
Ikiwa mambo yatakwenda kama yalivyopangwa Arsenal hadi kufikia Jumatano jioni inaweza kuwa imesajili wachezaji wasiopungua watano.
Wachezaji wengine ambao Wenger amewaulizia wa timu zao ni pamoja na Yosi Benayoun na Frolent Malouda wa Chelsea. Chelsea wanataka milioni 7 kwa Benayoun na milioni 10 kwa Malouda na kama wachezaji hao wanapenda kuendelea kuishi London basi kuna uwezekano wa kumsajili mmoja wao.
Come on Arsenal! bado pesa ipo ya kutosha.
Tutaendela kupeana updates.