Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Octopus yule jamaa ni mido kweli kweli

Katika pass 7 maybe mbili ndio back pass
Anaweza kucheza tough na soft touches

Nilishawai kuandika, Kama unataka uone ubora wa martinel, saka, odegard
Basi mtu mweusi partey akae pale dimbani awafanyie kazi chafu
hamis77 alifikiri Jorginho kaja ili Partey aondoke. Tukamwambia huyo jamaa ni hatari
 
Arsenal's next five premier league matches, how many points will we get?

Chelsea
Sheffield United
Newcastle
Burnley
Brentford
 
hamis77 alifikiri Jorginho kaja ili Partey aondoke. Tukamwambia huyo jamaa ni hatari
Hapana sikuwahi kufikiri hivo, najua kabisa Jorginho aliletwa kwa short term ndio maana alipewa mwaka mmoja na nusu ,Main target alikuwa Caicedo Kama unakumbuka baada ya Brighton kukomaa HAUZWI ,ikabidi tutafute Short term yenye quality Zaid ya Lokonga

Jorginho mechi hiz za Carabao ,FA cup Ni nzuri kupatia matokeo ,maana kwa Quality yake Ni Zaid ya Casemiro .

Ukitaka kujua u smart wa biashara angalia manjesta wanaenda kununua DM mwenye miaka 31 kwa €70m

Arsenal wananunua DM mwenye miaka 31 kwa €12m
 
JE ARSENAL YA MWAKA HUU IMEIMARIKA KULIKO YA MWAKA JANA

Arsenal are currently two points better off this season compared to the same fixtures last year.

Compared to the corresponding league matches in 22/23, #AFC have:

  • Scored 16, down from 19 in 22/23
  • Conceded 6, compared to 8 in 22/23
  • Won 20 points, up from 18 in 22/23
    20231008_125823.jpg
 
𝐓𝐎𝐍𝐘 𝐀𝐃𝐀𝐌𝐒 𝐍𝐀 𝐉𝐈𝐍𝐀 𝐋𝐀 𝐌𝐑 𝐀𝐑𝐒𝐄𝐍𝐀𝐋 𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐃𝐀 𝐉𝐄𝐋𝐀 •

Maisha ya wanasoka yamekuwa na simulizi nyingi sana za kustaajabisha na kufurahisha, unamfahamu yule beki bora wa Arsenal na Timu ya Taifa ya England?

Moja wapo ya mabeki hodari sana enzi hizo alikuwa ni Tony Alexandar Adams ambaye aliweka utawala mkubwa zaidi kwenye soka la England hadi kuwekwa kwenye kumbukumbu (Hall of Fame) kutokana na mchango wake mkubwa katika soka.

Tony Adams anajulikana kama mchezaji ambaye amezaliwa kwaajili ya kuiongoza Arsenal ( baada ya kuwa Nahodha wa Timu hiyo zaidi ya miaka 14), lakini kama haitoshi maisha yake yote ya soka ameichezea Arsenal pekee.

Adams alisajiliwa na Arsenal akiwa kijana wa shule mwaka 1980 akiingia kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tarehe 5 Novemba 1983 dhidi ya Sunderland katika Idara ya Kwanza, wiki nne baada ya siku yake ya kuzaliwa ya 17. Adams amekuwa mchezaji wa kawaida msimu wa 1986-87, akishinda kombe lake kuu la kwanza msimu huo wakati anacheza katika ushindi wa Mwisho wa Kombe la Ligi ya Soka dhidi ya Liverpool huko Wembley.

Pamoja na Lee Dixon, Nigel Winterburn na Steve Gould, Adams alikuwa sehemu ya "FAMOUS BACK FOUR" ambao walipiga mstari katika ulinzi wa Arsenal, ambao chini ya George Graham alikuwa maarufu kwa matumizi yake ya nidhamu nzuri ya mtego wa kuotea.

Umaridadi wake uliompa jina la MAN MARKING/STOPPER huku akiichezea Arsenal zaidi ya michezo 670 ndani ya miaka 20 huku akiiongoza kama Nahodha ndani ya miaka 14 iliwafanya wakina IAN WRIGHT kumpachika jina la MR. ARSENAL ambalo ndiyo hufahamika nalo, lakini DAVID O'LEARY ndiyo mchezaji pekee anayeshikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi kwenye Historia ya Arsenal ( zaidi ya michezo 700).

Licha ya Ubabe wake uwanjani, Tony Adams alikuwa mlevi wa kupindukia na mkorofi zaidi kwenye kumbi za starehe, alikuwa akiripotiwa mara nyingi akitoa vichapo kwa watu kwenye Nightclub baada ya kulewa.

Mwaka 1990 aliipeleka jela baada ya kuwa na kesi ya kugonga gari aina ya FORD SIERRA sababu kubwa ilikuwa akiendesha gari huku amelewa, anachukuliwa kama mwanasoka mwenye hadhi kubwa Duniani ambaye amebobea kwenye uraibu wa pombe.

Adams amehamishia soka lake kwenye ukocha akifundisha timu kadhaa kama Granada ya Uhispania. Nilimkumbuka sana MR. Arsenal chini ya kocha bora sana CHAPMAN. Enzi hizo.

SALIBA is Another TONNY in BackLine? Namuona kabisa.

Zingo sports
 
𝐌𝐀𝐑𝐓𝐈𝐍𝐄𝐋𝐋, 𝐀𝐋𝐈𝐕𝐘𝐎𝐊𝐀𝐓𝐀𝐋𝐈𝐖𝐀 𝐎𝐋𝐃 𝐓𝐑𝐀𝐅𝐅𝐎𝐑𝐃 •

Kama walivyo mastaa wengi kutoka Amerika ya kusini ikiwemo, Roberto Firmino, Antony, Gabriel Jesus wanatokea katika familia maskini ambazo hazikuwa na uwezo hata wa kuwapeleka shule.

Haikushangaza upande wa Gabariel Martinell alikuwa miongoni mwao, amezaliwa kijiji cha Guarulhos huko São Paulo ambacho kilikuwa kinasifika kuwa na wakazi wasiojiweza kimaisha, mzee wake Joåo Martinelli aliendelea kupambana ili Gabriel asome akiamini ndiyo sehemu pekee itakayompa maisha na kuiokoa familia yake. Lakini ilikuwa tofauti.

Maisha ya Martinelli yalianzia katika Academy ya Corinthians, lakini yeye alipendelea zaidi kucheza mpira kuliko kusoma, wakati anaendelea na masomo yake, mitaa ya Guarulhos iliitazama miguu ya Martinelli kama kivutio kikubwa kwenye jioni za mpira wakiamini anakipaji kikubwa.

Siku moja kocha wa Timu ya Academy anayosomea alimualika kufanya majaribio kwaajili ya kuona kitu kipaji chake, Martinelli alionyesha kipaji chake kama hatacheza tena na kupewa nafasi kwenye klabu ya Corinthians.

Maisha yake ndani ya Corinthians yalikuwa bora sana baada ya kufunga jumla ya mabao 202, aliweza kuwavutia ITUANO FC ambao walikuwa wakishika nafasi ya nne kwenye Ligi ya Brasil. Kwanini Manchester United?

Baada ya kusainiwa na ITUANO FC (2015) aliendeleza moto wake zaidi ya kuzivutia klabu kubwa kama Fc Barcelona, Real Madrid na Manchester United kumualika kufanya majaribio.

Wakati anafanga majaribio na Man United mara nne katika awamu tofauti akiwa na matumaini ya kusajiliwa, ilikuuwa tofauti baada ya kuambiwa hana nafasi ndani ya Old Traford.

"Kiukweli nilifanya majaribio mara nne Man Utd nikiwa na miaka 13, 14, 15 na 16. Nikiwa kwenye mazoezi ya klabu hiyo nilikutana na wachezaji wa Timu kubwa kama, Zlatan, Paul Pogba, Wayne Rooney na Evra.

Lilikuwa tukio ambalo sikufikiria kama nitakutana nalo kwenye maisha yangu ya soka, niliweza pia kucheza na wachezaji kama Mason Greenwood".

Wakati anaondoka uwanja wa Carington, Martinelli alikutana na PAUL POGBA na kumuuliza, vipi kuhusu majaribio yako na utachezea klabu gani hapo baadae?. Martinelli alimuelezea kwa unyonge kukataliwa kwake ndani ya Man United baadae alimruhusu wapige picha pamoja.

Baadae alitua LA MASIA pale FC Barcelona kwaajili ya mualiko wa majaribio lakini hakufanikiwa baadae alirejea ITUANO huko kwao Brasil. Baadae wakala wake alimuuliza, vipi kuhusu Arsenal?..

Majibu ya Martinelli yalikuwa rahisi sana baada ya kumwambia hakuna jibu lingine ni wakati wa kuelekea London, wakati huo Jopo la mascout wa Arsenal walikuwa wanafuatilia kiwango cha Martinelli.

Mwaka 2019 Arsenal walimsajili Martinelli kama U21 ambaye atakuja kufanyiwa majaribio ya kupandishwa timu ya wakubwa.

Note: Martinelli alipelekwa academy ya Arsenal Hale End akakutana na kina Saka,Smith Rowe,, alicheza michezo kadhaa ya U21 Kama academy wa Arsenal , hivo Martinelli huwa anahesabika pia katokea Academy ya Arsenal

TUENDELEE SASA

Lakini wakati huo kulikuwa na vigezo kwa vilabu vya England kumsajili mchezaji kutoka Amerika ya Kusini ambavyo Martinelli alikuwa navyo kutokana na kuwa na Uraia wa Italia akiwa na paspoti kutokana na mzee wake kuwa ni Muitaliano.

Hii ilimsaidia kusafilri na timu kwenda Pre Season sehemu ambayo alienda kufanya makubwa, baadae alipandishwa Timu ya wakubwa akipewa nafasi ya kuonyesha alichonacho.

Baada ya kusaini mkataba na Arsenal kutokana na umaskini wa Familia yake, aliichukua Familia yake na kuja kuishi nayo London, Baba yake alikuwa na hofu kama wangeweza kuishi London kutokana na kiwango cha mwanae.

Baada ya Martinelli kuingia kwenye kikosi cha kwanza zilikuwa ni furaha kwa familia yake huku akiifungia klabu yake mabao muhimu kwenye nyakati tofauti. Hadi leo Gabi ameingia kwenye kikosi cha kwanza na anaitumikia Brasil kwenye National Level.

Good luck Gabi.

Zingo sports
FB_IMG_1697125896477.jpg
 
David_Ornstein:

"Kwa upande wa bei na wasifu, sioni Arsenal ikimnunua Osimhen. Ninahisi yuko kwenye orodha yao, . Wingi wa washambuliaji wenye ubora kwa sasa ni mdogo kiasi kwamba klabu yoyote kubwa inayotaka kumsajili huenda ikawa inasoma majina yale yale - Osimhen, Martinez, Ferguson, Sesko, Boniface n.k.

[@TheAthleticFC
 
𝐓𝐎𝐍𝐘 𝐀𝐃𝐀𝐌𝐒 𝐍𝐀 𝐉𝐈𝐍𝐀 𝐋𝐀 𝐌𝐑 𝐀𝐑𝐒𝐄𝐍𝐀𝐋 𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐃𝐀 𝐉𝐄𝐋𝐀 •

Maisha ya wanasoka yamekuwa na simulizi nyingi sana za kustaajabisha na kufurahisha, unamfahamu yule beki bora wa Arsenal na Timu ya Taifa ya England?

Moja wapo ya mabeki hodari sana enzi hizo alikuwa ni Tony Alexandar Adams ambaye aliweka utawala mkubwa zaidi kwenye soka la England hadi kuwekwa kwenye kumbukumbu (Hall of Fame) kutokana na mchango wake mkubwa katika soka.

Tony Adams anajulikana kama mchezaji ambaye amezaliwa kwaajili ya kuiongoza Arsenal ( baada ya kuwa Nahodha wa Timu hiyo zaidi ya miaka 14), lakini kama haitoshi maisha yake yote ya soka ameichezea Arsenal pekee.

Adams alisajiliwa na Arsenal akiwa kijana wa shule mwaka 1980 akiingia kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tarehe 5 Novemba 1983 dhidi ya Sunderland katika Idara ya Kwanza, wiki nne baada ya siku yake ya kuzaliwa ya 17. Adams amekuwa mchezaji wa kawaida msimu wa 1986-87, akishinda kombe lake kuu la kwanza msimu huo wakati anacheza katika ushindi wa Mwisho wa Kombe la Ligi ya Soka dhidi ya Liverpool huko Wembley.

Pamoja na Lee Dixon, Nigel Winterburn na Steve Gould, Adams alikuwa sehemu ya "FAMOUS BACK FOUR" ambao walipiga mstari katika ulinzi wa Arsenal, ambao chini ya George Graham alikuwa maarufu kwa matumizi yake ya nidhamu nzuri ya mtego wa kuotea.

Umaridadi wake uliompa jina la MAN MARKING/STOPPER huku akiichezea Arsenal zaidi ya michezo 670 ndani ya miaka 20 huku akiiongoza kama Nahodha ndani ya miaka 14 iliwafanya wakina IAN WRIGHT kumpachika jina la MR. ARSENAL ambalo ndiyo hufahamika nalo, lakini DAVID O'LEARY ndiyo mchezaji pekee anayeshikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi kwenye Historia ya Arsenal ( zaidi ya michezo 700).

Licha ya Ubabe wake uwanjani, Tony Adams alikuwa mlevi wa kupindukia na mkorofi zaidi kwenye kumbi za starehe, alikuwa akiripotiwa mara nyingi akitoa vichapo kwa watu kwenye Nightclub baada ya kulewa.

Mwaka 1990 aliipeleka jela baada ya kuwa na kesi ya kugonga gari aina ya FORD SIERRA sababu kubwa ilikuwa akiendesha gari huku amelewa, anachukuliwa kama mwanasoka mwenye hadhi kubwa Duniani ambaye amebobea kwenye uraibu wa pombe.

Adams amehamishia soka lake kwenye ukocha akifundisha timu kadhaa kama Granada ya Uhispania. Nilimkumbuka sana MR. Arsenal chini ya kocha bora sana CHAPMAN. Enzi hizo.

SALIBA is Another TONNY in BackLine? Namuona kabisa.

Zingo sports
Tierney alienda kuanzisha ugomvi nafikiri dhidi ya West Bromwich nafikiri Guendouz au Xhaka wakaenda kumzuia Adams akasema timu haina umoja kwanini hawakumsaidia Tierney kumpiga mchezaji wa West Brom 😆
 
Partey
Nimemsikia huko zenzychenko anahojiwa akaulizwa kati ya partey na rodri nani mkali akasema partey Rio akataka kubisha,amemtolea analysis nzuri sana,amesema rodri ni mchezaji wa system wakati partey ni mchezaji mwenye quality anafit kokote,akamwambia Rio kama anabisha aje amtazame Partey wakiwa mazoezini
Thomas partey ni fundi haswaaa
 
Tierney alienda kuanzisha ugomvi nafikiri dhidi ya West Bromwich nafikiri Guendouz au Xhaka wakaenda kumzuia Adams akasema timu haina umoja kwanini hawakumsaidia Tierney kumpiga mchezaji wa West Brom
 
Shida pia magoli yetu tunayasambaza hafungi mtu mmoja mfano tungekua na mtu ambaye kwa wastani kila mechi ana xG ya 1.9 au 2 ingekua rahisi. Sasa sisi xG hiyo ipo kwa timu nzima
Ndio Maana Ian Wright kamwambia Arteta amlete Toney pale mbele

Tunahitaji mtu mwenye xG kubwa ,ametolea mfano mechi na Spurs amesema tulichezea Sana nafasi
 
Back
Top Bottom