Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Huyu jamaa ni mzigo kabisa sijui tulimsajili kwa kazi gani hasa. Alafu Arteta kamng'ang'ania hatari.
ZittoJr ,kuna kipindi ulisema Rice bado hajai. Master ile DM inamshinda na mimi nilikubaliana na wewe, ila kwa nilichokiona toka game na Wale Seleman (Nyumbu) had game ya leo PSV nimekubalo kua Rice ni Dm Pure kabisa na kaiweza kui master vzr kwa aslimia zote

Vipi kwa upande wako Rice bado haiwezi ile DM?
 

Mkuu huyo Flano ameamua tu kunichafua, Mimi sio chawa wa mtu

By the way Kai anahitaj ku-adapt as soon as possible
 
 
Wakati Xhaka anacheza ilikua timu ikipata mpira anaenda kuhold kushoto kwenye mid ili kutoa support kwa Martinelli au kumpa chance Martinelli ya kuoverlap.

Kisha timu ikiadvance anakua nje ya box. Kutegemea na attack anaweza na yeye akaingia kwenye box au akaendelea kubaki hapo. Kwakua Xhaka hana mbio nahisi hakua anarisk kujisahau kuingia kwenye boksi kwakua angeshindwa kurecover.

Pia Xhaka alikua anatoa pass kushoto, kulia, mbele na nyuma.

Kai timu ikipata mpira instinctively unamuona anazama deep kwenye next phase ya attack kwamba sasa ushamuona anaenda mpelekee mpira au ucheze naye 1 2.

Ila Kai hana vision. Siyo mzuri kwenye accuracy ya pasi lakini pia kwa timu yetu na jinsi yeye anavyoanza kukimbia namna pekee anaweza zicheza 1 2 ni ama iwe counter au amuone Odegaard upande wa kulia anavyoushughulikia. Ile instinctively kukimbia mbele wenzake wanashindwa kumpa mipira kisha mtazamaji naona anafanya iwe ngumu kugewa mpira muda goli linatafutwa na kuona jamaa anakimbia pasi.

Timu imepiga jumla ya pasi 520 katika hizo Kai ni amegusa mpira mara 45 tu na imemfanya awe wa mwisho. Pia ndiye aliyepoteza mpira mara nyingi.

Kuna mshkaji kamuuliza zitto junior kwamba kwa Rice ulisema hivi na vitu kama hivyo.

Yaani shabiki anaona uvivu kucounter hoja hivyo anaamua kukuletea ukumbusho kumaanisha kwamba ulishawahi kukosea once so hata hapa hauwezi kua sahihi. Zitto naye akianza kufukua vitu kuonyesha kwamba alishawahi kua sahihi hata mara 100 hua mnakasirika.

Timber kacheza mechi moja na wote tukasema hapa tuna mtu.

Rice ananunuliwa kabla ligi haijaanza nikasema kumuuza Partey kisa Rice kaja ni risk, wabaki wote kwanza kipindi Rice anazoea mazingira. Well game ambazo Partey alikuepo tukakubaliana humu kua kweli Partey ilibidi awepo ili Rice azoee polepole.

Wakati tunasema hivyo Rice hakua mbaya, ila hakua anafanya alichokifanya kuanzia game ya nne (hesabu kuanzia ya City) ile siku jamaa alionyesha upande mwingine kabisa mpya na ndiyo yupo nao mpaka mechi ya mwisho mimi kuona.

Rice ameadapt fasta. Timber kaja na kuonyesha haimsumbui kukaa kule kulia. Kai bado anajitafuta, ndiyo kusema hatutakiwi kusema kua jamaa anajitafuta? Hata sisi tusiposema takwimu zinasema. Kila game zitaonyesha mchezaji kafanya nini, akifanya sawa watu wakibisha takwimu zitasema pia.
 
Kwa performance hii ya Raya

Ndugu yangu Aaron Ramsdale ana kazi ya kufanya ,

Angalia hizo claims , angalia Raya alivyo mzuri kudaka Kross ,

Aaron Ni mbovu kwenye Kross ,mech na Fulham hakutokea kufata mpira wa Kona tukafungwa goli

 
So far wanataka mchezaji afeli ,hii Tabia wameitoa kwa mashabiki wa nyumbu

Ila ukishajua Kai anatumikaje Arsenal Wala hutaingia kwenye hiyo mitego

Kai am, Trossard,rice,Vieira wanacheza LCM but kila mmoja ana majukumu tofauti na mwenzake

Mfano Kai majukumu yake acheze LCM lakin awe Kama second CF,


Jana kaanza mechi Kama LCM kamaliza Kama false 9

So Kai ataendelea kucheza sababu anatimiza majukumu yake vzr tu

| Mikel Arteta on Kai Havertz playing different roles in the game:

“He was very connected today in the game. It’s true that I ask him to play in two different roles in regard to the opponent’s behaviours. He’s so intelligent the way he does it. It’s just finishing one or two actions that we had again, but it’s coming and he’s so willing to do it.”

[@arsenal]
 
| Mikel Arteta on how hard it is to compete in the Premier League and the Champions League:

“Winning always helps and when you see that dressing room and how happy they were today at the end, if tomorrow I tell them to train they will train, for sure.”


[@Arsenal]
 
Kipind kile Onana anahusishwa kuja Arsenal sikumtakaga kabisa aje ,

Aliwa cost Ajax mechi vs Spurs nusu fainal wakashindwa kwenda fainal ,

Ni kipa pazia ,mzuri miguuni tu

Huwa nacheka Sana nikiona mashabiki wa nyumbu wanadai Onana anamzidi Aaron Ramsdale,

Onana kwa timu based possession ingemfichia mapungufu mengi, ila kwa timu za ujanja ujanja atapigwa Sana

Shots 12 Goals 9

Ukicheza na manjesta jitahidi kusaka On target tu magoli mtapata

Kuna pazia lingine Sanchez wa Chelsea,,
 
Jana nimemuangalia, alicheza vizuri
 
Mikel Arteta:

"Emotionally, winning is the best, the best, the best.

It is the best thing you can do, and I now have 24 players desperate to play on Sunday." [Arsenal]
 
Msimamo Ni ule ule tutamaliza group na points 15-18

Round 16 tutakutana na kiazi


UCL tutaanza rasmi Robo fainal tukisubiri opponent ambao bado sion Ni tishio

Ukweli unabaki pale pale mpinzani mkuu UCL Ni Mancity

Wengine unga unga mwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…