Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Hii ni 2020

Baada ya kusema usajili wa Partey ulikua panic buy na kutabiri tutakua hovyo kwenye attacking tukaanza kuchezea bakora nikaja andika hiki kiishu.

Nimesahau tulitoka kupigwa na nani ila ilikua timu ya kawaida.
Ukiachana na majerui yake
Unahitaji partey auzwe?

Partey defensive
Odegard attacking

Odegard na H. Auor wote ni attacking. Yani xhaka au elneny ndio wawe defensive mid yetu?
Umesahau nyekundu za xhaka zilikua zinatokea akicheza wapi

Kama utafukua makaburi utakukatana comments za watu ikiwemo na Mimi tulikupinga Sana hili
Kinachotucost partey ni majerui tu
Ambapo msimu uliopita hakukaa Sana nje
 
Wachezaji wa nje hua hawajibu hovyo.

Mitoma baada ya kumgalagaza Arnold akaulizwa anamuonaje akajibu ana nguvu tofauti na anavyoonekana
 
Unaniuliza kwakua nimewahi kusema auzwe au unataka ona nasema nini?

Kwa mwaka ule tulikua hatuna AM.

Ila DMs walikua wawili.

Partey alivyokuja wakawa 3

Na bado hatukua na AM. Naelewa mpango ulikua aje AM na DM

Tukifukua makaburi nitakuta mnapinga na mtakuta nimeandika kwamba Partey atatuimarisha defensively na siyo kwenye kushambulia. Its the reason vipigo vyetu vilikua 1 au 2
 
Tumekubali kwa Brighton yameisha hatuna cha kujitetea , tusubiri zamu yenu msimu uliopita mlikula 3 nil so usicheke sana tena pale pale emirates.
Kwni tulivyoenda kwao walitufunga au tuliwafunga🤠🤠🤠....manenomaneno meeeengiiii 🤠🤠🤠...ww bdo ni WA kawaida sana mkuu....mna wachezaji machachari sio wazuri....ukitaka kulielewa hlo siku mkikutana na Chelkenge ndo utaelewa....maana itakuwa machachari dhidi ya machachari 🤠🤠🤠
 
ndugu yangu hamis77 usikimbie jukwaa banaa jana tulikua tunatania tu, tunakusubiri utupe mchanganua wa leo jinsi mtakavyompiga nyumbu, tumemiss kusikia kutoka kwako mambo ya pressing na overloading, aerial duel, kuinterchange na kuinvert kiungo.
Tunatamani kusikia kutoka kwako jinsi Kai leo atakavyonyumbulika.



#Arsenyo Ndoo
#Kai Kiatu
 
Nyukesto mna misimu miwili kwenye ligi au Inonga (Mkongo) uliopakiwa jana umekuchanganya mzee
Anajitoa ufahamu....yaani anakimbilia kwny kichaka hawakuwa na hela ukimuuliza kwni sisi tulikuwa nazo kpndi hko....anarukia tena twenti yiaz no ipielo taito...ukimuuliza nyny mna mangapi tangu mpira uanze kuchezwa....anakaa kimya🤠🤠🤠
 
Mtapigwa mpk mchakae🤠🤠🤠
 
This is 2020

Tunatembelea vipigo watu wamekimbia jukwaa na hapa ni member akielezea
 
Kwa kipindi kile defensive ya xhaka na elneny ilishafeli
Ata wangekuwa defensive wanne dizain hizo, lakini tupihitaji defensive iliyokua Bora

Kuhusu kipindi kile Kumbuka tulikua tunajenga timu, Bora tuanze kuimalisha defensive
Kikawaida ata huku mchangani kwenye kuita timu, huwa tunapanga mabeki viungo wakabaji then washambulia

Kumpata partey, xhaka anachukua majukumu ya #8

Namba 10 ndio akavutwa odegard

Sasa unasemaje panic usajiri wa partey?

Tena ilikua haina Mambo mengi, ni kuweka mzigo kumchukua mchezaji. Mchezo umeisha, ndio maana haukua na rumors nyingi

Alafu dili la H. Aour lilikua na usanii Sana
 
Mbona tulishajua juu ya drama la dili la Aouar na kwanini Arsenal tuliachana nalo?

Panic buy ni usajili unafanywa ili kutuliza mashabiki, yaani haijalishi kulikua na longo longo ama la. Tuliwahitaji wote wawili AM aliwekwa wazi ila DM akawa hatajwi mpaka Arsenal tukaenda kuweka video yenye code kumaanisha anakuja mfaransa na mghana.

Ila akaja mghana peke yake on deadline day
 
Mtapigwa mpk mchakae
Unaongea huku unaogopa, leo ni matchday halafu mpaka muda huu Msemaji wa Arsenyo kwa ukanda wa Afrika Mashariki ndugu yangu Mc Masingeli hajaonekana humu jukwaani mpaka muda huu halafu wewe bado tu hujashtuka kua leo kitawaramba?
Mwenzio Masingeli machale yameshamcheza mapema kua leo litawakuta jambo ndio maana kaamua kujipiga ban 14hrs before game, humu Masingeli ataonekana miezi 3 baadae.
 
Najaribu kukuelewa kuwa tuliwahitaji wote

Partey na H.Aour
Ambao hao ni wawili

Tukaja kumpata partey, ambae unasema ni panic

Then tukamvuta odegard
Kwaio tukawa tuna partey na odegard. Nao ni wawili idadi ile ile

Badala ya Aour akaja ni Odegard

Sasa shida ilikua wapi hapo?
 
Hebu kumbuka vizuri.

Partey na Odegaard nani alianza?

Halafu Odegaard alivyofika alianziwa wapi?
 
Nakubaliana na wewe kwenye hili na players wengi wa Africa sio wa kweli kwenye mambo ya umri unaweza kuta Partey ana 36-38 but kwenye football anasema umri wake 29 kama Essien kipindi kile tatizo kubwa sana hili
 
Kitu ambacho huwa kinaleta utofauti kati yetu ni either kushindwa kuelewa au kusahau kama mpira ni Sanaa, na Sanaa siku zote haina specific formula.

Namaanisha nini, namaanisha kwamba kwa mfano wakati ndg Castr anaona tatizo lipo kwa viungo washambuliana yupo mwingine anaona kwamba tatizo la viungo washambuliaji linaanzia kwa viungo wakabaji na hivyo hivyo hata kwenye kusolve kila moja atasolve kwa kadri anavyoliona tatizo na finally wote mnakuwa mmesolve tatizo.

Lkn pia kuna kitu kingine ambacho ni watu wachache wanacho na pia kinatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine ambacho ni UWEZO WA KUONA KUTAFSIRI NA KUGUNDUA TATIZO hapa sasa ndo huwa professionalism inahusishwa. Kwahiyo kuna wakati lzm tukubaliane kutokukubaliana lkn pia tukubali kujifunza kutoka kwenye michango ya vitu ambavyo hatuvijua kwa kurudi field (kufuatilia mechi na sio kutizama mechi) . Ndg Castr na Will Jr ni miongoni mwa wanaotoa michango mizuri ya kufuatilia mechi mengine yaliyobaki kwao ni ya Kibinadamu

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Hii haiwezi kua mechi ya kwanza mzee.

Odegaard alikua na tatizo la kusita kushuti. Sidhani kama kipindi ana hili tatizo klaa mechi za kwanza awe na hiyo rating
Nakupa kazi Sasa nitafutie kikosi kana hivyo mechi ya odegard iwe ligi au Europa
Nikiona yupo position tofauti na hiyo


Hiyo changamoto Ni kweli alikua anayo, na hapo amekuja kwa mkopo
Alivyorud Madrid Arteta alikuhitaji hivyo hivyo

Hapo ndio watu wakaibuka kwanini tusimchukue Madison au buendia?
 
This is 2020

Tunatembelea vipigo watu wamekimbia jukwaa na hapa ni member akielezea
Mkuu, sijajua upo na point ipi inayofanya ufukue makaburi.

Ila ninalojua, hata mkibaki wawili humu jukwaani, haimaanishi wengine wamecha kuisapoti Arsenal.

Tupo mtaani kila siku, kila games za Arsenal tunaangalia. Tunafurahi tunaposhinda, tunaumia tunapofungwa.

Msijipe umuhimu sana kwa kuwa mpo active humu. You and me, we are just fans tuu mkuu.

Wadau, watoe mawazo tofauti tofauti bila kutishwa.

cc Flano
 
kikubwa kuwe na uhuru wa kutoa maoni sio watu wachache wajimilikishe jukwaa, pia members wajitahidi kukubaliana katika kutokukubaliana, humu kila mtu ana mawazo tofauti kulingana na upeo wake, unapolazimisha members wote wakubaliane na hoja zako ndio kunapelekea mgawanyo, chuki, kudharauliana na kuanza kutukanana wenyewe kwa wenyewe humu.
Pia members wajitahidi kuheshimu mawazo ya wenzao hata kama wanatofautiana kwenye mitazamo, mtu umemkosoa mara moja, mbili lakini bado anang'ang'ania msimamo wake achana nae endelea kujadiliana na wale ambao mitazamo yenu inafanana, haina haja ya kumuita mtu majina mabaya kisa tu mnatofautiana kwenye jambo moja.
Nyinyi kama mashabiki ya Shenalii mnapohitilafiana katika jambo moja juweni kuna mambo 100 yanayowaunganisha, sasa kwa nini hilo jambo moja mnalo tofautiana mnalipa nguvu ya kuwatenganisha kuliko yale 100 yanayowaunganisha?

Huu ni ushauri tu kutoka Unyumbuni lakini haimaanishi jioni tutawasamehe, kipigo chenu leo jioni kiko palepale Kima nyie


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…