Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Lakini pia naangalia Chelsea kuanzia leo...kutokana na watu waliochukua na aina ya uchezaji wao utakavyokuwa...hasa hasa kiungo chao
 

Another shit
 
I see.

So idea yako ya unpredictability itatusaidia mpaka wapi dhidi ya City,

Dhidi ya Brighton

Dhidi ya United
 
Wilson, murphy,barnes et vyuma?
hao wanamtoa nani kwenye best 11 pale Epl zaid ya kwenda tott ambayo ndo kwasababu keane hayupo tu,
 
I see.

So idea yako ya unpredictability itatusaidia mpaka wapi dhidi ya City,

Dhidi ya Brighton

Dhidi ya United
Mfumo unaokuja nao na aina ya wachezaji unaotumia katika siku husika...ize tu...uliangalia ile mechi ya Community shield...ile ndo proper example....kwa dk 60 nzima hawaku establish shot yyte on target...attempt zao zilikuwa nadhani 3 on target kwa mechi nzima...ya John Stones...lile goli na ile nafasi ya Foden alookoa Ramsdale...tungeenda kwa mazoea ya siku zte ile mechi tungetupa taulo mapema sana kwa sababu City ni wakatili kwlikwli
 
Wilson, murphy,barnes et vyuma?
hao wanamtoa nani kwenye best 11 pale Epl zaid ya kwenda tott ambayo ndo kwasababu keane hayupo tu,
Na kuna mtu anaitwa Willock anaye...hyu bwna mdgo alikuwa arsenal tukawauzia....ndo maana jana nilikuwa namwqmbia ndugu yangu level zake ni kina Aston villa huko
 
Game time ya Murphy mchango wake ukiviweka kwenye mzani na Fabio Vieira vitakushangaza alf unachukulia poa bench la Arsenal ilo ilo bench la Arsenal ndo liliingia likasababisha City apaki basi na kuchomolewa goal juzi tu hapa au unajisahaulisha kaka?
 
Ukisoma uchambuzi wa George ambangile instagram utaelewa leo Mikel kafanya nini ambacho hatukufanya last game ikatucost.

Nimeshindwa tu kuucopy uchambuzi wake.
Mfumo mzuri but poor choice of players, Kuna wakati Partey alikua ana overlap kama RB. Hii ni hatari hata goli lilipitia upande wake maana sio natural RB so lazima azidiwe.
2. Kamuanzisha white na Saliba ilihali natural LCB kama Gabriel na Kiwior walikua benchi.
3. then Harvetz was a poor choice bora angeanza na ESR pale kati.
4. Nketiah hakupaswa kuanza au walau angeondolewa half time, Trossard alipaswa kuanza tungeshinda hata 5.
5. Then sub zilichelewa sana dakika almost 70!! Why?

I support Arteta ila asipo tibu makosa ya msimu uliopita ya kushindwa kumanage mchezo basi atatucost
 
Humu ndani vipi mbona mnashikana mashati wenyewe kwa wenyewe, mmeshinda sasa mbona vurugu humu naona kuna watu humu hawataki timu ikosolewe na wengine ni wakosoaji.

Sasa mbona mapema sana wazee
hapo ni forest sisi kama fans tunawaambia tulieni mfurahie ushindi maana siku zinakuja huko mbele mtakimbilia mafichoni, aliye na jezi ya arsenal auze anununue leso maana itakuwa vilio na kusaga meno
. Wengine watataka arteta asulubiwe na wengine wakihangaika kumfanya awe mfalme pale viunga vya emirates.

Back on pitch mnalalamika nini kwani chances jana mme create ngap? Mpaka mtake magoli zaidi ya 3 first half ? Utoto wenu ni ule ule wa pass nyingi zisizo na maana so nothing new. Kuna timu huko tumempiga mtu mkono na bado chance za kufunga zilikua zaidi ya 5 tupo tunawasubiri wazee wa ku overload and kufanyeje sijuii.

Tulikubaliana arteta anarusha jezi juu atakayeokota jezi ndo anaanza sasa partey jana kaokota jezi yenyewe position as right back na wengine wote so tusilalamike ndivyo arteta ameamua kurusha jezi juu watakaokota ndo hao wanaanza na hii ni kutokana na quality na squad mlio nayo si mnajua nyinyi ni most valuable squad in the world right now.

Kuna dog la arsenal linaitwa win kumbe surname yake ni nothing


First name: WIN
Surname: NOTHING
WIN NOTHING to boost morale of the team.
 
Game time ya Murphy mchango wake ukiviweka kwenye mzani na Fabio Vieira vitakushangaza alf unachukulia poa bench la Arsenal ilo ilo bench la Arsenal ndo liliingia likasababisha City apaki basi na kuchomolewa goal juzi tu hapa au unajisahaulisha kaka?
Aisee umenikumbusha , Bench la Arsenal

Fabio Vieira,Trosaard ,Smith Rowe ,City walipaki Basi wanaomba mpira uishe

Iliwekwa formation ya 3-1-6
 
Kila mfumo huendana na wacheza maalumu
Shukrani mkorea kwa Mwaliko, hamis77 we Jamaa nakuwaga interested na Comments Zako, Nimeona Michango Mingi ya waja Huku kuhusu Game ya ArsNott, Honestly hakuna kipya nje ya last Season Game ambayo Arsenal wanapoteza 1-0, ile Game Partey alianza nafasi aloanza Game ya jana na kati walikuwa Xhaka, Jorginho, Ode, CB's Kiwior, Gabriel na White. So kiuhalisia kama amekuja na Mfumo Ule ule alopoteza nao Game, na sababu kubwa ya Arsenal kupoteza ilikuwa kichwani zaidi kuliko habari za Mifumo tofauti wakati ule kwa Arsenal Notts walikuwa na World Class GK in Navas!

Mimi naungana na baadhi ya wachangiaji kwenye Uhitaji zaidi wa Arsenal{CB na CF} Fergie alishapitia mambo mingi mpaka kufikia hatua ya kusema "Attack wins you Games, Defense wins You Titles" Pep na sifa zote karibu Madirisha yote huwa anaboresha Def na sasa kaleta lile Jini Josko {Hapa wengi mtasema kuhusu Timber but Arsenal ukitoa Saliba wanaomkaimu Ubora unapungua sana, Injury yake Imewacost Ubingwa, Jesus anaumia lakini Gari Ars lishawaka na still timu inapata Matokeo, Zile Big Figures Nyuma hazina cha maana akikosekana Saliba} Timber Mchezaji na nusu but anapenda sana Duels kwa EPL kuwa salama season yote Ni kudra tu,

ARS players wengi walikiri kabisa ile kukosa Title ni mentality zaidi, Hapa Experince inafanya kazi zaidi, kama ARS ingekuwa na Mwalimu kariba ya kina PEP, KLOPP et al, wangekuwa na Title mda huu. Leicester walijikuta nafasi ambayo hawakuitegemea wakianza season, ilibidi uzoefu wa kina Ranieri ufanye kazi zaidi ya Uwezo wa Players,

Kuna kitu ki1 nakionaga sana kwa walimu wenye asili ya Kispanish, "EGO" Pep alikuja akataka tuaminisha angeiweza EPL Bila Natural CF, Na aliweka sababu nyingi kwamba Aguero haezi Press, Mwisho Kun ndo alimpa mataji karibu yote, amekuja pata Treble baada ya kusajili CF. Ila awali alituteletea kina Nolito, akaanza amini kina Negredo and Co. Luis Enrique alishndwaga Roma na Celta hivyo hivyo, Case yake Barca ni tofauti {Hakuna mwalimu wa daraja la kati mpaka juu angeshindwa chukua kila kitu na Neymar, Messi na Suarez tena wakiwa kwenye Peak yao} Enrique kachukua Spain anawaacha Alcantara na kina Ramos, hata kama asingewapanga wale washazoea mataji wanajua jinsi ya kuhandle Pressure, hana cha maana kafanya nayo,

Narudi kwa Mikel, Huyu jamaa ana Potential ya kuwa the Best Manager kwa kipindi kifupi kinachofata, ila asipotoa "EGO" wako naye wenzake na yeye ni mhanga anayo, ARS Inahitaji CB wa kiwango na CF wa uhakika then inakuwa ni Force haswa, mana City unaweza wabana ila Haaland anaweza kufunga hata 3 ndani ya dk 20, ukitaka makombe unatakiwa kuwa na watu hawa, Jesus mchezaji na Nusu ila unakuwa na Plan B ya kina Nketiah ni uongo,

Nahitimisha kwa Suggestion za mimi ARS ilimtaka sana Dusan Vlahovic, Bei yake ishajulikana sasa Pauni 45~60 unajibebea, then unakuwa na Beki mwingine wa kati mwenye Uwezo wa kueleweka Pembeni ya Saliba, hapa nadhani wa Bei za kawaida na ubora juu kuna Nico Schlotterbeck, Facundo Medina au Bastoni.

Mikel Game ya mwisho ya Msimu ulopita ilikuwa Emotional sana kwake na Mashabiki hata kuongea ikawa tabu Emirates, Fans walikuwa wana-Applauds karibu dk na zaidi, Sababu aliwafanya waamini tena, alizidi malengo ila msimu huu wanaamini wanaweza ni mapema sana but ARS inahitaji CF wa maana kuwa Force kamili, Msimu huu wanaamini tuna kitu ila karata ni za kuchanga vyema mana mashindano anakuwa yote ni ya Maana huwezi sema unapotezea moja kubaki na lingine kama ilivyokuwa kwa Europa, kwa sasa Emirates kamziki cha Ligi ya Mabingwa katasikika.
Inatosha waja naomba Kai iwe mada ya wakati Mwingine!
 
Ile unpredictabiliy ya ngao ilitugea chansi ngapi za kuscore?
 
Ile unpredictabiliy ya ngao ilitugea chansi ngapi za kuscore?
Nafasi tatu you can say...mbili alizipata Kai ila hakuwa clinical...na moja deflection iloleta goli...na hao ni City ambao hutegemei utawa dominate kipndi chote tofauti na timu zingine kwny ligi
 
Game time ya Murphy mchango wake ukiviweka kwenye mzani na Fabio Vieira vitakushangaza alf unachukulia poa bench la Arsenal ilo ilo bench la Arsenal ndo liliingia likasababisha City apaki basi na kuchomolewa goal juzi tu hapa au unajisahaulisha kaka?

Fabio viera huyu huyu ama? Yaani wewe viera anaweza kuingia na ukaona impact yoyote kweli nitajie game moja tu last season ambayo unaona viera alikua ana impact kwenye timu? Huyo hata robo ya willock dogo janja wenu wa zamani hafikiii.
Mkuu mchezaji mwenye impacts kwenye sub zenu ni trossard pekee hao wengine wapelekeni leeds then mtafute strong sub players , hatutaki kuwaona kwenye mateso mnayopitia GWK1 tayariii mshaanza kutafuta mchawi ni nan wakati sisi tumekuja 4 pale juu ya table
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…