Ukiwasikiliza sasa mashabiki wao unabaki unacheka tu, kuna mtoto wangu wa 4years asubuhi kila nikiwa natoka nyumbani hua ananiambia jioni nikirudi nimnunulie gari, pikipiki, baiskeli na meli, mimi hua naumuitikia tu halafu jioni nikirudi namletea pakti ya karanga au mahindi ya kuchoma.
Huyu dogo akili zake hua nazifananisha na mashabiki wa Arsenyau, utasikia dirisha hili tunamsajili Caisedo, Rice, Gundogan, McCallister hua nabaki kucheka tu maana najua mpaka dirisha linafungwa wanaishia kununuliwa karanga au mahindi ya kuchoma tu.