BUILDUP MONSTERS

Umeiona Ile Pasi ya William SALIBA kwa Granit Xhaka kwenye bao la pili la Arsenal? Tena kwa kutumia mguu wa kushoto? World class

Ile ndo Sababu Arsenal ni team bora EPL kwenye kujenga shambulizi Kuanzia nyuma.Ili ujenge shambulizi vizuri kuanzia nyuma unahitaji (A) Uwe Wana wachezaji ambao wapo vizuri mpira ukiwa mguuni kwao.Arsenal Ina Saliba, Gabriel,Ben White, Zinchenko, Ramsdale.

Lakini pia Lazima kuwepo na Muundo mzuri wenye virutubisho vyote kuwezesha ujenzi Bora wa hilo shambulizi.Arsenal mara nyingi wanajenga mashambulizi Muundo ukiwa 3+2.Gabriel , SALIBA na White+Thomas Partey na Zinchenko

Hata hivyo wakati Mwingine Inategemea na team pinzani inapeleka wachezaji wangapi kufanya Pressing? Kwa mfano kwenye hili bao, Fulham walifanya Man to Man Pressing kwa Sekunde 30.Maana yake walipeleka wachezaji 6 , Mitrovic akiweka Pressure kwa Ramsdale.

Lakini bado Arsenal walifanikiwa kutoka, unajua Kwanini? Position ya Granit Xhaka ule upande wa kushoto ikawa sehemu maalumu ya Arsenal kutoka kwenye Presha ya FULHAM (Out ball)

Hata dhidi ya team bora zenye Muundo mzuri kwenye kuweka presha ndani ya EPL kama Manchester City Bado Arsenal wana uwezo wa kujenga shambulizi kuanzia nyuma Bila wasi wasi na kufanikiwa

Nini umuhimu wa kujenga shambulizi kuanzia nyuma? (A) Kuufungua kwa urahisi Muundo wa kuzuia wa team pinzani.Kwanini? Kwasababu sio rahisi sana kwenye team kwenda kufanya Pressing Halafu bado Muundo wao kwenye kuzuia ukabaki umeungana.Lazima Kuna mashimo mengi mnaayacha nyuma.(B)Kuipa team Muundo mzuri wa kushambulia kwa utulivu na pasi za uhakika
FT

English premier league FULHAM 0-3 ARSENAL
Note; Umeshawahi kusikia neno HAT TRICK OF ASSIST? Muulize Leandro Trossard,nitamleta Baadae
View attachment 2547896