MARCH 1 2023 ,ni siku ya kutafuna Kile Kiporo chetu dhidi ya EVERTON.
-Mechi ya kwanza tulifungwa 1-0, Everton walikaa sana chini na Sean Dyche aliijaza sana Midfield ikiwa na Idriss Gana, Abdoulaye Dacoure ,Amadou Onana
-Everton walizuia kabisa Chanzo Cha hatari nyingi za Arsenal kwenye kutokea maeneo ya Pembeni kwa kuhakikisha Gabi Martinelli na Bukayo Saka hawapokei mpira wakiwana na 1v1
-Newcastle United pia walitumia approach hyo hyo na wakapata 0-0
-Mikel Arteta anatakiwa kuja na Solutions Leo,ili kutanua wigo wa Points dhidi ya Manchester City na kuwa 5
-Je anaweza pengine kuanza na Kieran Tierney kama Left back badala ya Zinchenko? Zinchenko amekuwa muhimu sana kwenye kuimarisha umilikaji wa Mpira wa Arsenal akisogea ndani pembeni ya Jorginho au Partey
-Lakini kwasababu eneo la katikati kurudi nyuma Everton itajaza sana watu, ufanisi pia wa Zinchenko unaweza usiwe wa Kiwango cha juu sana.Na kushambulia kupitia pembeni inaweza pengine kutoa majibu kidogo
-Kuanza kwa Kieran Tierney itamaanisha pia Gabriel Martinelli kuwa na uhuru zaidi kushambulia box kuliko akiwa anashika ule mstari wa Pambizo
-Kuna swali pia kuhusu Thomas Partey na Jorginho kuanza pamoja Leo.Kwangu naona mtu pekee anayeweza kufanya kile Granit Xhaka anafanya akisogea juu ni Fabio Viera.
-Vipi kuhusu Leandro Trossard na Eddie ENKETIAH? Eddie arejee kikosini au Trossard aanze kama mechi iliyopita?
View attachment 2533946