Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Azam FC ya ulaya
1676524531109.jpg
 
Haters wamejazana hapa lakini mimi bado ninaona arsenal akibeba ubingwa. Hiki ni kipindi cha mpito na kinaelekea mwisho.

Pia ni lazima Arteta akubali kufanya mabadiliko, Saka, Odegaard, Xhaka, Martinelli, Magalhaes, Partey, White na Saliba wametumika sana, awapumzishe.

Sasa ni wakati wa kuwaweka akina kiwior, nelson, esr, kt, tomiyasu, cedric, trossad, jorginho na vieira kuanza kwenye game zijazo.

Afundishe kupiga nje ya box na kuanzisha mfumo wa kuweza kupiga counterattack. Mfumo wa sasa kuingia mpaka ndani ya box umeshafeli.

Mashabiki wa arsenal mlioanza kutukana mnaonyesha ukosefu wa ukomavu na kutoufahamu mpira vizuri.

Good days are coming.
Awapumzishe akina nani??
Utajikuta relegation zone brother.
 
lembu eti kwamba unaona newcastle ndio inamchallenge zaidi arsenal kuliko city?!!

Ulikuwa unawajaza ujinga hawa ndugu zako.
 
Bado huwezi kukata tamaa ya Ubingwa eti kisa tumefungwa na Man City, mbona na yeye aliweza kupoteza dhidi ya Spurs, Liverpool, Man Utd ambao sisi tumeweza kuwafunga?
Man City kapoteza michezo 3 sawa na Arsenal na still ametuzidi mchezo mmoja zaidi.

Kuna mdau humu, alishauri tuongeze experienced striker mmoja pale mbele kuweza kuwa challenge Man City na wapinzani wetu wengine pamoja na kupata depth ya kikosi, lakini wenye timu hawakuona umuhimu. Sisi hatukuwa na nafasi ya kufanya chochote as hakuna anayetoa hela zake mfukoni kununua wachezaji na kulipia mishahara zaidi ya wenye timu.

Bado naamini ni mapema sana kukata tamaa, fanyeni ulinganifu wa Arsenal ya mwaka jana ilipocheza michezo 22 ilikuwa na alama ngapi kulinganisha na Arsenal ya mwaka huu iliyocheza michezo 22 sasa ina alama ngapi?

Iwapo tutajipanga bado tuna nafasi ya kushinda EPL, ligi bado hii Wakuu💪

COYGs
 
Sasa yale mashati yenu kama waganga wa kienyeji yataanza kupungua mtaani.

Mnatakiwa kujifunza toka jukwaa la man utd,siku tukifungwa tunampa heko mpinzani,tunajikosoa na tunaendelea na safari. Lakini uku arsenal jukwaa limejaa wajuaji kumzidi hata arteta na bench zima la ufundi kisa mchezaji mmoja kukosea mara moja.

Mwaka 2003 zilibaki mechi 8 arsenal akiwa anaongoza ligi kwa point 15 dhidi ya man utd ila hadi msimu unaisha,man utd akawa bingwa wa epl. Historia huwa haidanganyi.
Mechi 8
Gape 15
Na bado wakakosa ubingwa

Bora niendelee kushabikia WAZEE fc ya ujiji sasa

Note
Wazee fc ya ujiji mchezaji mwenye umri mdogo kabisa ni kipa ana miaka 56
Ila hii tunu haijawai kupoteza mechi yoyote toka 2010 mpaka jana wamemchapa mwandiga fc goli 4
 
Arsenal Fans sioni sababu za kukata tamaa, kwasababu Arsenal bado ana nafasi nzuri zaidi kuliko Man city kuchukua ubingwa kama wakiwa serious na wakiacha papara na utoto. Ingawaje ni kazi ya ziada inahitajika na wala si ya kitoto. Through game moja mkononi na kurudi kwa Gabriel Jesus naimani kitaongeza kitu kuanzia dressing room mpaka uwanjani. Wachezaji kama Eddie Nketiah, Reiss Nelson na Folarin Balogun si wachezaji wakuja kuibadilisha Arsenal kule mbele hata wawepo kwenye form gani. Ni aina ya wachezaji potential ku-generate fund kwenye timu Kutafuta wachezaji wazuri ambao determination yao ipo juu. Hata huyo Balogun anaonekana kuwika huko ufaransa huu ndio wakati Arsenal kupiga pesa kuachana na nao. Hizi mishe za kitoto za kuwaamini hawa consistently - immaturity player ndio huwa zinakuja kuigharimu Arsenal kila siku..
 
Back
Top Bottom