Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Yupo slow hawezi kutrack back hii inasababisha timu iwe vulnerable kwenye counter.

Akiwa na mpira anatumia muda mkubwa kuangalia team mates positioning hii husababisha anyang'anywe mipira mara nyingi ili kuepuka hili amekua aki-back pass.
 
Unyama sana mkuu!!!!
Wakati huo Martinelli akichoka, Trossard huyooooooo. Huku ESR akiendelea kuimarika zaid.

Moto wa hii round inayofata, ni zaidi na tuloanza nao!!!!Maji yataitwa mmaa!!!
 
Kama huna akili ya kuuangalia mchango wa mchezaji mpaka umsubiri kocha hilo siyo kosa langu
 
Nadhani kimbinu ni ngumu kuwatumia wote 3 kwa pamoja japo inawezekana. Sababu zangu binafsi ni kwamba;

1. Jorginho ni mzuri sana kwenye kupiga pass na anakaa vzr sana kwenye eneo lake. Shida yake ni kwamba hana uwezo wa ku-cover eneo kubwa akiwa peke yake kama DM hivyo kucheza pamoja na Partey au na Zinny itamfanya awe bora zaidi.

2. Partey kwa sasa ni kiungo (DM)alietimia na sifa yake kubwa ni uwezo wa ku-cover eneo kubwa ndo maana huwa anatumika kwa kusimama peke yake(single pivot) lkn nadhan kwa kumpunguzia kazi Arteta akamfanya Zinny kucheza km kiungo pia.

3. Zinny pia ni master kwenye pass lkn ana udhaifu kwenye kuzuia.

Kwahiyo kwa concept hiyo Partey anaweza kucheza pamoja na Jorginho kwa vile Jorginho anaweza ku-offer kile ambacho zinny anaki-offer kwenye kiungo na ikiwa hivyo maana yake ni kwamba Zinny itabidi ampishe Tierney ili kuimarisha ulinzi. Huu ni mtizamo wangu mimi
 
Ndicho nilichofikiria ,maana Jorginho namfahamu hawezi ku cover eneo kubwa ,Arteta anatumia Single Pivot Kama Pep au Barcelona


Ndio maana nikaona tukiwaweka wote na Partey plus Zinny

Nataka nione Nini kitatokea ,
 
USARA ZANGU GWIJI LA HIGHBURY

🤏
JORGINHO signing kwanini ni Usajili ambao atleast unatupa walau asilimia 60 ya tulichokuwa tunahitaji CM hapo mimi nitajikita kwenye tactical aspects

Wachezaji aina ya JORGINHO kwa sasa ni wachache mno watailano wanawahita REGISTA ni wachezaji ambao wapo vyema kucheza kama Orchstator au tuseme ball carrier kutokaea kwa mabeki

🤏
Kwa misingi hii hawa wana footwork nzuri na accuracy kubwa kupiga pass mahala sahihi na zikafika kila angle ya uwanja kwa misingi hii kwa vile Arsenal ni team ambayo ID yao ni possession based football basi Jorginho anafit

🤏
Kwenye soka kuna kitu tunaita press resistance wachezaji ambao hawana pressure na mpira ata wakikabwa ni rahisi kupata upenyo kuwa press uwa ni ngumu mfano Zinchenko sasa Jorginho type hiyo

kwa vile Arteta anahitaji kiungo anaecheza 6 awe ball carrier mzuri sio kukaba tu basi Jorginho anafit hapo sababu team ina miliki mpira muda mrefu

Wasi wasi wa watu wengi ni pindi team ikiwa haina mpira wanakaba vipi basi Nikupe siri watu siku hizi wanakaba ndani mfumo na sio mtu mmoja tu

Ukimuangalia Rodri au Bisquet ni Viungo kariba Jorginho ila bado team zao ni dorminant kwenye aspects zote

🤏
Naelewa Tumemkosa Caceido ambae pengine angekuwa long term replacement ya kina partey Lakini Nature deal imegoma kwa muuzaji swali tungeendelea tu na Partey bila walau cover

🤏
Jorginho 31 bado ana miaka 2 mitatu kutumika kwenye kiwango kizuri tu ndio maana team imempa short term deal ili kumuangalia 18 Months

Nimalize kusema Aliyepush kumsajili uyu ni Arteta aliwahi kukikili viungo wachache sana kariba Jorginho ndio maana alimuhitaji akiwa City hivyo anajua Ni set up gani atamtumia bila kuharibu balance ya team kiushambuliaji na kiukabaji

Mchezaji yeyote akivaaa jezi Arsenal namsupport 100% uyu ni mimi

Amigo adios hermanos
 
Yupo slow hawezi kutrack back hii inasababisha timu iwe vulnerable kwenye counter.

Akiwa na mpira anatumia muda mkubwa kuangalia team mates positioning hii husababisha anyang'anywe mipira mara nyingi ili kuepuka hili amekua aki-back pass.
Umekaa kijiweni umepiga zako mihogo ya buku na chai ya mia unakuja unasema humtaki jorginho bro tutafutie mchezaji wako unayemtaka wewe tupelekee arsenal watu wanatoa hela sio matako
 
Yupo slow hawezi kutrack back hii inasababisha timu iwe vulnerable kwenye counter.

Akiwa na mpira anatumia muda mkubwa kuangalia team mates positioning hii husababisha anyang'anywe mipira mara nyingi ili kuepuka hili amekua aki-back pass.
Hivyo ndivyo watu hubishana mkuu kwa maana km kuna aliye tofauti na wewe atakuja na mtizamo wake kisha mwenye strong reason ataonekana amechambua vzr na wengine watajifunza.

Mfano mimi ninachokiona kwa Jorginho ni kutokuwa na uwezo ku-cover eneo kubwa hivyo anapojisahu tu kidogo anajikuta yuko vulnerable kwenye eneo lake lkn ebu chukulia kukiwa na mtu mwingine wa kumsaidia km Zinchenko au wakicheza wote wawili na partey km double pivot?

Kitu ulichokisema ambacho mimi nakubaliana na wewe ni kwamba hatujawahi kuwa na bahati na wachezaji wanaotoka Chelsea
kwahiyo hata kwa Jorginho inaweza kuwa same story
 
Kila team huwa na malengo katika suala zima la usajili na kila kwenye usajili huwa Kuna target ya kwanza na target ya pili na ya tatu

Nikikazia sana kwenye hili dirisha dogo la January target ya kwanza ilikuwa ni Mudryk
Ila iliposhindikana target yetu ya pili ikawa Trossard tukampata

Tukahamia kwenye kiungo hapo target yetu ilikuwa ni Caicedo Brighton wameweka ngumu kwamba hawamuuzi licha ya kutuma ofa mpaka 80M

Bado wameipiga chini tukageukia target ya pili Kwa Jorginho na sio mbaya tumempata bado mnaanza kulalama

Iko hivi hakuna dirisha gumu kwa mchezaji kama kumuuza kama dirisha dogo kwa sababu klabu nyingi huwa zinakuwa nusu ya malengo ambayo wamejiwekea

Na hata kama wameamua kumuweka sokoni basi gharama zao zinakuwa kubwa sidhani kama yule Mudryk angefika thamani ya 100M au Leo Caicedo kufika thamani ya 80M sio kwamba hawajui mpira wanaujua sana

Ila ni kwamba kwa dirisha dogo kama hili wachezaji wa hizo level ni wachache tofauti na dirisha kubwa ambapo wachezaji wanakuwa wako wengi sokoni na kunakuwa na muda mwingi wa kutafuta replacement za wachezaji wanaowauza

Jorginho na Trossard ni wachezaji wa malengo mafupi tofauti mtu kama Zichenko au Jakb na ningewaona watu wa maana humu ndani basi mngeanza kulalamika kipindi kile Cha dirisha kubwa

Kwamba mnahitaji replacement ya maana ya Partey na mlikuwa wa kwanza kuwasifia na kuwatetea wakina Lokonga na Elneny na kuna watu walisema ingekuwa ukichaa kutoa 45M kwa Douglas Luiz Leo tumepeleka 80M na imekataliwa

Dirisha January ni gumu sababu wachezaji wanakuwa Wana gharama kubwa na pia kulingana na sera za klabu yetu ni wagumu kumwaga pesa

Mnaoponda usajili wa Jorginho tukutane May mponde vizuri tumekosa ubingwa Ila kwa sasa wote tusimame kwenye mstari mmoja kama mlivyokuwa mnaniambia Mimi tumuamini Arteta


#COYG
#ONCEAGUNNERALWAYSAGUNNER
 
Yupo slow hawezi kutrack back hii inasababisha timu iwe vulnerable kwenye counter.

Akiwa na mpira anatumia muda mkubwa kuangalia team mates positioning hii husababisha anyang'anywe mipira mara nyingi ili kuepuka hili amekua aki-back pass.
Pass 8000 zote back pass, anakeraa huyo mwamba.
 
Jorginho is such an Arteta player. He is great in a team that plays on his strength. He has a manager's brains and will be perfect for Arteta because his football IQ is so high. That's why Pep wanted him at City when he was at Napoli and why Arteta already wanted him last summer.
 
Ila na wewe ndugu kama unapenda ligi hivi!.. unamfuatilia sana jamaa na unafukua Hata maubisha I yenu ya miaka mingi ya nyuma.. kama unaona hakuelewi busara ni kukaa kimya na kuendelea kutoa mchango wako chanya humu..
 
Arsenyani mnatakiwa mchukue darasa hapa, tuition Chelsea.



Endeleeni na wachezaji wenu wa mafungu, watu wanavunja vibubu. Mudryk, Enzo. 🔥 Kuwa club kubwa siyo kuongoza ligi, kuna msimu Leicester pia alikuwa bingwa.
 
Umekaa kijiweni umepiga zako mihogo ya buku na chai ya mia unakuja unasema humtaki jorginho bro tutafutie mchezaji wako unayemtaka wewe tupelekee arsenal watu wanatoa hela sio matako
Niliondoka humu muda mkubwa nimerudi nakutana na hizi species zinazoishi maeneo ambayo matako ni currency, huna akili huwezi hata fikiria kama na mimi naishi maeneo kama yako au hapana.

Mimi kijiweni nimeshinda sana ila siyo siku hizi nigga enzi za mimi kushinda kijiweni ni zile Arsenal haijielewi. Jitahidi kitu kimoja toka kwenye hiyo lifestyle utaharibiwa wewe bado mtoto mdogo, stress za matokeo yako ya form four usiniangushie mimi. Mimi hili jukwaa nakuja kwa kupenda siyo kwakua sina kazi za kufanya, na kama unahisi matako yako yanaweza tumika kufanya malipo confirm tuone tunafanyaje.
 
Jamaa hawezi cover eneo kubwa kwakua yupo slow, now kuna viungo at their peak walikua slow na mambo yanaenda mfano Busquet alichokosa kwenye speed akacompensate katika technical ability na skills na kwakua timu yao inafanya sana possession hii trait haikuwahi mfanya aonekane mzigo.
 
Arsenyani mnatakiwa mchukue darasa hapa, tuition Chelsea.

View attachment 2502001

Endeleeni na wachezaji wenu wa mafungu, watu wanavunja vibubu. Mudryk, Enzo.
Kuwa club kubwa siyo kuongoza ligi, kuna msimu Leicester pia alikuwa bingwa.
Leicester alikuwa bingwa akiwa na wachezaji wenye viwango kama Mahrez (alikuwa mchezaji bora wa msimu) Ngolo Kante, Vard, Schemical
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…