Mkuu hizi ni short term plan...! Arteta anaangalia kila uwezekano wa kuendelea kubakia katika mbio za ubingwa, kwahiyo kwenye shida anajaribu kuziba kwa wakati
Ndio alichokifata kwa Trossard baada ya kumkosa janjaro aliekimbilia Chelsea, na sasa baada ya kuhisi kumkosa Moises ameona bora aangalie mchezaji ambae atakuja kuleta impact ya moja kwa moja kwenye timu
Mimi kama Arsenal fan nitafurahi tukimpata jamaa maana ataongeza kitu katika first eleven kama atapata namba na pia ataleta hali ya kujiamini kama ilivo kwa Zinny na Jesus maana jamaa ni winner
Kama atakuja nahisi atapewa mkataba wa miaka 2 maana najua hawezi kukubali mwaka mmoja, lakini pia kwa mkataba wa miaka miwili inakuwa ni nzuri zaidi kwake lakini pia kwa team