Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mie ni mshabiki wa Arsenal, nimeangalia yale magoli yanavyorudi nikaona mtu unaweza kuzimika ghafla. Ukweli watu hawawezi kubadilisha timu, ila kuwa mpenzi wa Arsenal inahitaji moyo saana. Leo nimeamua kucomment maana kila siku huwa nachungulia halafu naugulia maumivu. Hata leo Arsenal hawa hawatashinda. Yaani itakuwa ni kuokota point moja moja mpaka ligi inaisha. Threat kwa MAN U ni Chelsea peke yake na si Arsenal. Ngoja niendelee na Spain kwanza. Afya muhim
 
...hayasemeki mkuu. Msimamo wa ligi mpaka sasa

1. Man United

2. Chelsea.

3. Arsenal

...najiskia kama nichukue likizo jukwaa hili mpaka August, msimu ujao!

Daaa pole sana mkuu...Lakini ndio mpira huo hamna jinsi....
 
Mie hapa nipo hoi, utasema adhabu kushangilia vijana wa wenger.


....I predict huu ndio msimu wa mwisho wa Arsene Wenger.
Nahisi hata sign Contract kuendelea. Baada ya Game ya leo matusi
ya mashabiki kuelekea kwake yatazidi maradufu!

 
Naona Modric kaangushwa refa kapeta...ila leo Atkinson amechezesha mechi vizuri to be honest.
 

Kumbe wewe unajjuwa......Usikate tamaa maana ndio upenzi huo mkuu haha...nunueni wachezaji wa experience na sio kutegemea watoto waje wachukue vikombe!
 
yani kocha wa arsenal kaishiwa kabisa ufundi

Mkuu Arsenal imejaa watoto tu ambao hawana experience sasa watategemea vipi kushinda??kocha naona kachoka sasa hivi na hajui nini anafanya
 
yani kocha wa arsenal kaishiwa kabisa ufundi

...Truth Hurts, lakini ukweli ndio huo.
Suala sio wachezaji, tactics pia zinachangia.
Well,...

....pamoja wakuu. Nilikuwepo!
 
Mkuu Arsenal imejaa watoto tu ambao hawana experience sasa watategemea vipi kushinda??kocha naona kachoka sasa hivi na hajui nini anafanya
Mkuu huwezi kusema hawana experience wakati wengi wao wamecheza kwenye top flight for two, three seasons or more.
 
Reactions: Mbu
Hahah nimemuona Wacha1 uwanjani, mmemuona huyo jamaa mwenye jezi ya njano ya Arsenal alikuwa anafuta machozi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…