Arsenal (The Gunners) | Special Thread


KSE have promised to provide £50m for January-23 window
 
Nilishasema wachezaji wa Arse88 wana nux, Xhaka anawaponza wenzie.
 
MNA UHAKIKA XHAKA NI MCHEZAJI WA KIWANGO CHA DUNIA?
 
Wachezaji w Arse88 wana nux. kila timu ya taifa yenye wachezaji wa Arse88 lazima watoke, kama hamamini leo England wanatolewa na senegal, Saka anawaponza wenzie.
WC ikishinda timu yenye mchezaj wa Arse88 wanaoanza kikosi ch kwanza,niitwe mbwa.
Jana ameingia tu Martinelly Brazil wakafungwa...
Leo kuna mmoja kaanza huku Switzeland ni mauaji..
 
Edo yeye anasemaje kwani?
Edo bhana alikuwa hamkubali Arteta mwanzoni,akiwa wasafi anasema aondoke tu, Kuna group tupo na kina madee ,Lile la Arsenal Tanzania, tulipambana Sana kuwaeleza process ya timu ,mwisho wa siku Edo akawa humuambii Kitu Tena kuhusu Arteta ,akajibatiza kabisa na cheo Cha RAIS WA ARSENAL TZ anasema atamrithisha mwanae hicho cheo .

Edo anasema anaamini katika mbinu za mwalimu na wachezaji waliopo .
 
Hata mimi nilikuwa naona Arteta anazingua, ila nimekuja kukubali maneno ya mentor wake Pep.
 
Mnarudi kulekule kwa zitto junior yeye alitamani tu kumuona Joao Felix anakuja Emirates kuziba pengo la Jesus ila akashambuliwa humu kama nyuki.
Hatujamkataa Felix , tulichompinga anaponda Sajiri za Arteta kumtaka Murdky na Danilo yule dogo wa Palmerias.

Kama mwalimu atamtaka Felix ,au hata Feisal Salumu aheshimiwe maana anajua atamtumia vipi

Felix Ni mchezaji mzuri na tunataman aje .
 
XHAKA AGOMEA MAPUMZIKO

Awali Mikel Arteta alisema wachezaji wanaotoka World cup atawapa mapumziko ya muda kabla hawajajiunga na timu Dubai .

Hali imekuwa tofauti kwa kiungo Granit Xhaka


Granit Xhaka anasema anasafiri kwa ndege hadi Dubai mara moja ili kujiunga tena na kambi ya Arsenal.

"Ligi Kuu(EPL) inanisubiri. Nilitaka kuwa hapa (WC) muda mrefu zaidi , lakini tulipoteza .
Nina furaha kurejea sasa na timu. Nina kitu cha kufanikisha huko (Arsenal)."
 
️Granit Xhaka -


Tunahitaji kumu
unga mkono Eddie (Nketiah) pia, kwa sababu atakuwa sehemu kubwa sana ya miezi miwili au mitatu ijayo.


(@TheAthleticFC)
 
Jorge Mendes amezungumza na Arsenal pamoja na Chelsea na United kwa ajili ya Joao Felix.

Atleti watahitaji €130m -€140m mwanzoni

Chanzo Ni (@MatteMoretto)



Habari nzima inasema Arteta na Arsenal wameulizia upatikanaji wa mchezaji huyo.


(@MatteMoretto) Ni Chanzo Daraja la 1(Tier 1) kwa habari za Atletico Madrid.

Sidhani kama kuna mtu analipa kiasi hicho Januari. Tusubiri tuone kitakachotokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…