
| Gabriel Martinelli:
"Nataka kushinda mataji, nataka kuwa mabingwa. Nadhani klabu, mashabiki na wachezaji tulionao, wanastahili kushinda kitu. "Na hiyo ndiyo ndoto yangu, kushinda Ligi Kuu, kushinda Ligi ya Mabingwa."

| Gabriel Martinelli kuhusu Vibe la mashabiki Emirate
"....... unapokimbiza mpira, na unahisi kuchoka unataka kukata tamaa ... mashabiki 60,000 wanaimba pande zote ... utaupata mpira huo. The energy boost is incredible."
unakumbuka mnamo Agosti wakati Saliba alipojifunga bao dhidi ya Leicester? Alikuwa anarudi nyuma huku akiwa na hasira, na labda mashabiki wengine wangemzomea. Lakini mashabiki wetu walishangilia. Walikuwa wakimuimba”
"Wao [mashabiki] walikuwa wakimwambia [Saliba baada ya kujifunga], 'Tuko pamoja nawe hata iweje.' Dakika mbili baadaye, tulifunga bao.
Hiyo ndiyo Arsenal.”
: "Tutaendelea kutafuta ushindi kila mchezo, ndivyo klabu hii inapaswa kufanya. Arsenal sio kuhusu ‘kupata pointi’. Arsenal sio kuhusu kumaliza nafasi ya nne. Arsenal inahitaji kupigania mataji, ligi, Ligi ya Mabingwa. Hicho ndicho ambacho mashabiki wanastahili.”
SAFARI YA KUJA ULAYA
Ninamshukuru Mungu kwamba nilikuja Arsenal mwaka wa 2019. Ninaamini sana kwamba mambo hutokea kwa sababu fulani, na nina furaha sana hapa.
Inafurahisha kutazama nyuma nilipotoka, kwa sababu ningeweza kuishia mahali pengine kwa urahisi. Unaona, niliwahi kuwa sehemu ya majaribio huko Manchester United. Kwa kweli nilikuwepo kwa majaribio kadhaa.
Nilikutana na wachezaji wengi wakubwa. Nilipokuwa na umri wa miaka 17, nilifanya majaribio yangu ya mwisho huko, kwa hiyo nilirudi Brazili nikingoja Matokeo.
Siku moja baba aliniita sebuleni. Alikuwa amezungumza na wakala wangu ..
Aliniambia Manchester United walikuwa wamesema hapana. Sio tu, "Hapana, kwa mwaka huu." Lakini, “Hapana, hatumtaki. hata kidogo.”
Kusema kweli, niliumia. Walikuwa wameniona nikicheza mara kadhaa katika Majaribio na nilikuwa na uhakika wangenisajili.
Wiki chache baadaye nilipata majaribio mengine, huko Barcelona. Nilitumia siku 15 huko. Hawakunitaka pia. Hilo lilikuwa rahisi kukubali, kwa sababu ilikuwa TRIAL(jaribio) moja tu, tofauti ya Kule Manchester United ambako nilifanya majaribio mengi….
Nakumbuka niliketi na baba yangu na kusema,
“Tutafanya nini?”
Nikurudi BRAZIL TU.....
Miaka kadhaa baadaye, Baada ya United kusema hawakunitaka
. Kwa bahati nzuri, mara baada ya hapo nilikuwa nikifanya vyema sana katika Copinha - Kombe la Vijana maarufu la São Paulo .
Ofa mpya zilikuwa zinakuja. Rafael aliponiambia kuwa Arsenal wananihitaji, sikufikiria mara mbili.
Nilimuuliza Baba, “Unaonaje?”
Alisema, "Twende London."
Hatua bora tuliyowahi kufanya.
MAISHA LONDON HAYAKUWA MARAHISI
Sikuweza kuendesha gari pia. Lazima uzungumze Kiingereza ili kupata leseni.
Nilitumia miaka miwili kupata usafiri au kuagiza Ubers. Unajua ni nani aliyeniokoa? Emi Martinez.
! Aliishi dakika 10 kutoka nyumbani kwangu, kwa hivyo alinichukua ili kunipeleka kwenye mazoezi na uwanjani. Wakati mwingine tungemchukua Dani Ceballos. Emi daima alijaribu kusaidia kila mtu. Wakati mmoja, hata nilitumia muda wa Mwaka Mpya nyumbani kwake na familia yake.
Pia nilipata usaidizi mwingi kutoka kwa David Luiz, mtu mwingine wa kustaajabisha. Bila watu kama hawa mwanzo wangu ungekuwa mgumu sana.
Nilichukua masomo ya Kiingereza mara tatu kwa wiki. Nilitazama sinema na mpenzi wangu. Ninampenda, lakini jamani, ananikera! Ingawa anatoka Rio de jenairo daima anataka kutazama kwa Kiingereza na mimi nataka kutazama kwa Kireno.
Lakini wakati ambao nilihitaji sana usaidizi ni nilipopata jeraha la goti msimu wa joto wa 2020.
Nilikuwa nikifanya mazoezi niliposikia maumivu kwenye goti langu.
Madaktari waliniambia nilikuwa nimeharibu gegedu(Cartilage).
Miezi mitano nje.
Nilitokwa na machozi. Sikuweza kuamini. Nilikuwa nimeteguka kifundo cha mguu hapo awali, lakini hii ilikuwa nusu mwaka bila kufanya kile ninachopenda. Sikuweza hata kuweka uzito kwenye mguu wangu. Lakini baada ya wiki moja nilijisemea,
"Hey, hakuna maana ya kulia. Tuendelee.”
Mnamo Desemba nilirudi. Basi nini kilitokea? Nimeumia tena!! Katika mwanzo wangu wa kwanza, kipa wa pili wa Man City, Zack Steffen, aliruka ndani yangu. Nilikuwa najizungusha kwa maumivu, ikabidi nitoke nje.
Bila shaka nilikuwa na wasiwasi. Bahati nzuri haikuwa serious. Wiki chache baadaye nilikuwa karibu kuanza dhidi ya Newcastle, na nilitonesha kifundo cha mguu wangu . Wiki nyingine nje.
Kwa hivyo kurudi kwangu hakukuwa rahisi kabisa.
Mikel amekuwa mtu mzuri kwanu kila wakati. Wakati sikuwa nikicheza sana msimu uliopita, nilienda ofisini kwake, na akanihakikishia kwamba nitapata nafasi yangu. Ninataka tu kucheza kila mchezo, unajua?
Hata nilipotoka sub dhidi ya Forest siku nyingine, nilisema, "Ah, ningependa kufunga bao lingine ...."
Lakini tuna michezo mingi. Naelewa. Nimefurahia sana kwamba nilichukua nafasi yangu nilipoipata. Naipenda sana klabu hii. Kikosi ni kama familia kubwa.
Sote tunaheshimiana sana. Ukituona kwenye mazoezi utaelewa kwa nini tunacheza vizuri, kwa sababu hata katika mchezo rahisi wa pasi hakuna anayetaka kupoteza. Nyumbani bado hatujapoteza pointi, kwa sababu hali ya msimu huu ni bora zaidi kuliko hapo awali. Wapinzani wanahisi presha kila wakati Emirates.
Chanzo
😛layer Tribune
Mtafsiri: Mimi
View attachment 2420976