Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Akibisha na hapa Basi Tena,
 
Huenda haangalii mechi , anasikia matokeo ,

Sisi mashabiki huwa tunakuwa na Wachezaji wetu wa mfukoni ,kocha anao wake ,anajua anataka achezaje ,

Pep alimtaka Cucullera akijua atamtumia vipi, Chelsea bila kuwa na DOF wakaingilia dili la watu kisa mchezaji ni mzuri ,wakambeba ,Sasa hivi wanadai Ni mbovu
 
Oya CR7 anawasagia kunguni

| Cristiano Ronaldo: ‘In my opinion it will be hard to imagine #mufc at the top of the game in the next 2-3 years.’ [@PiersUncensored]
Christiano alishatumbukia nyongo United baada tu ya kushindwa kufuzu kucheza Uefa.
Management ilivyomkazia kuondoka ndio wakazidi kutia ndimu kwenye kidonda.
Kwa alichokifanya + kiwango alichonacho kwa sasa sidhani kama atapata timu yoyote ya maana, labda aende zake Marekani au Uarabuni akapige hela.
Binafsi nilikua namkubali na kumtetea sana Ronaldo ila tokea alivyozingua kipindi cha pre-season amenitoka kabisaaaaaa.
 
Sa kwanini nikudanganye ndugu yangu

Nimemess up hapo kwenye timu. Ni Bologna siyo Fiorentina.

Na bologna alikua RCB.

Niles amewahi cheza lB na sababu ni hiyo ya dominant leg kulia ni rahisi kudefend dominant leg kushoto.

Mechi ya Liva Tierney akihojiwa alisema hakupangwa 'sababu za kimbinu'

Yaani ni kwamba he succesfully plays kama LB lakini huyu ni makeshift LB hatuwezi sema tuna LB watatu na yeye akiwemo. The only reason hachezi RB ni kwakua White amekua consistent mno na hiyo nafasi ambayo White aliianza baada ya Tomi kua majeruhi
 
Confirmation that the tournament Arsenal will be competing in during the World Cup break will be called the Dubai Super Cup.

They will play Lyon (Dec 8th) and AC Milan (Dec 13th), but not Liverpool.
 
Unabishana na hizo data? Leta data zako kuthibitisha usemacho, Hajacheza mechi na Liverpool tu Kama LB , Ndio maana tunasema UNATUPANGA , ,

akiwekwa LB anakuwa compact Zaidi kimbinu sababu anatumia both feet ,huyo Niles alikuwa anawekwa mech moja tu,

Lakini Tomiyasu unaweza kumuweka LB Msimu mzima ,

Takwimu zimewekwa hapo zinakuonyesha amekuwa akicheza hizo nafasi Zote za backline ,ungekuja kubisha kwa Hoja na takwimu ungeeleweka .

Arteta mwenyewe anakwambia alimsajiri sababu anacheza nafasi Zote hizo ,wewe unadai kacheza LB mechi moja..


Mikel Arteta on Tomiyasu’s ability with his weaker foot:

“When we followed the player, it is one of things that I came across & it gives you a lot of solutions. He can use both feet, he can play right centre-back, left centre-back, left-back. That gives you enormous variability.”

Kwa MUJIBU wa Arteta huyo kwake Ni LB,RCB,LCB,LB



Mikel Arteta says Takehiro Tomiyasu is so comfortable using his left foot that the Japan international could play anywhere along the Arsenal backline.
 
Cr7

"One day i walked into Erik Ten Hang’s office unannounced and i caught him red handed..
Him, Rashford and Sancho, he was forcing Sancho and Rashford to call him Arteta and forced Rashford and Sancho to call themselves Martinelli and Saka respectively.
There and then i knew there is no football club here"- Cristiano Ronaldo


 
Hizi Troll tu watu wanajitungia ,
 
Hivi vikomedi vya kutunga ndiyo vinafanya dunia izunguke 😀
 
Kwa kawaida neno Xg huwa lina maanisha expected goal from chances created. Ex. Chelsea (0.24) 0-1 (2.38) Arsenal.
Wolves (0.48) 0-2 (2.18) Arsenal.

Xg is determined from position and situation of the shot. stat zinaonesha tunaongoza kwenye Xg difference, Xg difference ni kama vile goal difference, unachukuwa xg created minus xg conceded, namba zinaonesha Arsenal is the best team kwenye kila aspect msimu huu.
 
| @FabrizioRomano:

"Kutokana na kile ninachoambiwa, Mudryk amekuwa akifurahishwa na nia ya Arsenal, sasa na pia Agosti. Anapenda klabu na mradi huo, na kwa hakika Arsenal wako kwenye kinyang'anyiro pamoja na vilabu vitatu au vinne zaidi." [@caughtoffside]
 
Arsenal hapa anatakiwa atoke na pointi si chini ya 13
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…