Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kuruka ruka ndiyo kawaida yenu ila cc huwa tunawafumua malinda tu
 
Waambie ukweli hawa wajinga, Arsenal ni timu ya masihara yn timu ina vitoto vitoto alafu ndio ije ichukue ubingwa wa ligi au UCL? Waambie wasahau
 
Hizi tambo ndio zimekuwa zikiwapoteza miaka yote ,
 
Unaota wewe ati
Ubingwa EPL ni wa City...
Nyie labda mkapambanie Carabao.
 
Weka takwimu tumewazidi kila kitu nyumbu
Hivi wewe jamaa ni mzima Kweli sasa timu inacheza ilu imzidi mtu au ipate ushindi inatakiwa mashabiki wa arsenal muanze kupimwa ubongo saizi.

Yani watu wanataka point wewe unaleta habari za kucheza mpira mzuri kwani kuna mwaka arsenal mjacheza mpira mzuri mbona toka kwa wenger mnachezaga mpira mzuri ila kombe la ligi sio muda mtatimiza miaka 20 mjabeba aise.
 
Weka msimamo basi tuone point zako ngapi after the Win.

stop making noises you peasants, still on top of the table though.
 
Aaaha Sasa na wewe takataka acha sifa Sasa ..kuwaponda arse8 siyo kwamba nyie mutakuwa mabingwa. Hapana, nyie bado Ni takataka tu Kama Hawa arse8 ..hapa bado hamuna timu ya kuchukua ubingwa.
 
Sasa kama anatawala possesion why uwaunderrate viungo wa arsenal?wakati mpira wametawala na bahati imeamua

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
Bahati!? Fuatilia jinsi United wanavyocheza na timu zinazo-possess. Jiulize kwanini United ana magoli mengi msimu huu dhidi ya Arsenal na Liverpool kuliko Southampton na Leicester City.

Mlizidiwa kimbinu na kosa kubwa mlilofanya ni kuja OT kusaka points 3 (ndiyo kila timu inahitaji points 3) unapaswa kujua aina ya opponent unayekutana naye. Kila mechi inapoanza timu inakuwa na point 1 ya uhakika hiyo ndiyo mlipaswa kuilinda suala la points 3 lilipaswa kuja mchezo utakapoamua opponent wenu akifanya errors.

Mawazo yenu mliyaweka zaidi kwenye kuendeleza winning streak yenu bila kujali mtatoka na nini OT. United wameshinda kwasababu ya defense, walichofanya goli la kwanza walicheza jinsi Ten Hag anavyotaka 'pasi nyingi' na goli la pili na tatu ni 'The United Way' mpira wa counter attack wakawaingiza kwenye mtego kwa kupaki basi kitu ambacho kiliwafanya wachezaji wenu wote kupanda kusaidiana kuifungua United na hapo ndiyo defense nzuri ilipoipa ushindi United kwa kutoruhusu goli.

Mlipopoteza mipira wakati mnashambulia ndiyo United kwa kuwatumia Bruno na Rashford wakawaadhibu kwa counter. Pasi za Bruno huwa ni hatari kwenye mipira ya counter attack.

Arsenal mngekuja kwa lengo la kupata droo huenda mngefaulu, mlipopata goli la kusawazisha momentum ndiyo ikawaingiza zaidi kwenye mfumo wa United maana mliamini sasa tupande wote tusaidiane kupata goli la ushindi, na ile sub ya Ronaldo iliwachanganya mabeki wenu huku wakimuacha Rashford anafanya mikimbio yake.
 
Wakati Bruno anatoa pasi ya goli la pili wachezaji 7 wa Arsenal walikuwa kwenye nusu ya uwanja ya United.

Goli la tatu wachezaji 8 wa Arsenal walikuwa upande wa United.

Na nafasi zote hizo mabeki wenu wameshindwa kucheza offside trap kwa kutokuwa aware uwanjani.
 
You have nailed it bro
 
AKILI KUBWA

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Aaaha Sasa na wewe takataka acha sifa Sasa ..kuwaponda arse8 siyo kwamba nyie mutakuwa mabingwa. Hapana, nyie bado Ni takataka tu Kama Hawa arse8 ..hapa bado hamuna timu ya kuchukua ubingwa.
Nyinyi mnayo, nakubali
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…