Moja kati ya timu yenye kikos finyu, Liverpool nae yupo
Ukiondoa ile starring 11 yake, bench hakuna watu
Katika hiko kikos chake cha kwanza. Wazee 90% na katika hao wazee pancha zipo za kutosha humo
Alcantara ndio pro pancha
Livekuku nisipo muona top4 wala sitashangaa
Man u, hii ni maiti ambayo jana imemng'ang'a muoshaji
Ukuta wa nyumbu una breach sana,
Jana bahati tu haikuwa upande wa liverkuku
Chelsea, huyu ni kama mgonjwa wa kichaa. Huwa kinatulia
Lakin muda wowote kinaamka(kupata matokeo mabovu)
City huyu ndio anatishia amani kwa sasa
Japo game alizo cheza so far
Sio yule city ambae anakutafuta kweli kweli
Haland ni finisher mzuri, lakin anapoza mashambulizi
Katika hizi game tatu, ARSENAL ameonesha kiwango kikubwa sana na mpira mzuri
Yani kila mchezo ni mzuri kuliko uliopita, hii inamaana gari linawaka kwenye mteremko
Arteta ni kocha wa mwezi as things stand
Liverpool na city wakiendelea hivi, basi watupe hilo kombe kuokoa muda
Come on you gunners
