Arteta aliipokea timu ikiwa Europa. Akaitoa nje ya top six ila ikarudi Europa kwa mlango wa nyuma. Kisha akashindwa kuifikisha Europa, CL na hata conference league.
Na msimu huu ameirudisha tena Europa.
Huku kikosi chake kikipoteza mechi 5 ambazo alitakiwa kushinda moja ili aende CL.
Tuhesabu tumefanikiwa? Anafaa kubaki kua kocha?
Mimi nafikiri anafaa lakini kuna maeneo anatakiwa kujirekebisha haswa katika kusajili, priority na namna anavyohandle wachezaji.
Tukianza katika usajili;
- Baada ya kua kocha akaazimia kupunguza upana wa kikosi ambacho kiliongeza wage bill ila performance ilikua hovyo. Akaachana na wachezaji wengine kwa mkopo, wengine free, wengine wakauzwa. Wakaondoka wakina Sead, Ozil, Iwobi, Auba, Bellerin, Guendouz, Torreira, Saliba, Mari, Mustafi, Nelson, Niles, n.k.
Kisha kiangazi akasajili Lokonga, Partey, Tavares, White, Martin, Ramsdale na Tomiyasu. Ilivyofika January akawa ana option ya kumsajili Melo na Kulusevski lakini akaona haina maana waliopo watamaliza msimu.
Ngwe ya pili ilivyofika katikati it was obvious kwamba timu haiwezi survive na Lokonga na Xhaka wakiwa kati ikabidi Elneny apate namba.
Wakati Arteta anakuja alimuambia Elneny hayupo kwenye mipango yake ni goli la Elneny la pre season ndiyo limembakisha Arsenal. Meaning kama asingescore Elneny asingekuepo na tungebaki na Lokonga na Xhaka pekee na tungejikuta tupo chini zaidi ya hapa.
Kisha unakumbuka kwamba amewaachia kwa mkopo Niles, Guendouz na Nelson wana uzoefu kuzidi Lokonga na ingekua sahihi angebaki na angalau wawili. Torreira simsemei sana kwakua alishasema anataka aondoke so isingekua na maana kumlazimisha abaki. So Arteta angeweza kubaki na Guendouz na Niles akamtoa kwa mkopo Nelson na pale kati bado tungekua tuna watu wanaoweza kusimama bila wewe kuhofia.