Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Nimekuelewa sana ndugu , nasubiria kwa Tammy
 
Kwani we jamaa umeona Winga wangapi wamekua AM? Wa kwanza Grealish, kisha kuna Buendia.

Sasa kuna ajabu gani Odegaard kucheza kama AM? Wakati namba yake ya asili ni Winga? Sijajua wapi huelewi, akiwa anasajiliwa Arsenal alisema kwamba anafurahia kucheza kutokea kulia (Namba ya Bukayo) ila anaweza kucheza kama AM na atasikiliza maamuzi ya kocha.

Mimi nikasema Odegaard siyo AM. Kwamba anadeliver haimaanishi yeye ni AM naturally. Hata timu ya taifa kuna mechi anacheza kama RW haswa Sorloth akiwa benchi au majeruhi ila Sorloth akiwepo ndiyo atakua RW na Odegaard anakua AM.

I hope utanielewa sasa.
 
Huyu niliwahi kumwambia hapa Arteta ameachana na 4-2-3-1 na Sasa anatumia 4-3-3 yenye double 8 , akanibishia bila fact kisa tu liverscore wameweka hivo

Now anadai Osmhen Ni mtovu wa nidhamu kwa red 1,
Nigga unatafuta kila angle siyo? Unahama tu.

Haya siku hizi Arsenal inacheza 4 3 3.
 
Aisee yaani tangu asubuhi mpaka mchana namuambia mtu kama price tag itakua juu haina haja ananikatalia ila kaambiwa same thing anakubali.

Sometimes watu wanaamka na watu humu.

Tujihadhari.
 
Odegaard Ni AM ndio main position yake kutokana na profile zake, Ni sawa Leo uniambie Saka Ni LB kwakuwa tu alicheza huko, Baada ya Arteta kukaa na saka akaona ana profile za RW ,na ndio imekuwa main position yake

Odegaard amecheza hizo LW na RW lkn Hana profile kubwa zakukupa matokeo ktk hizzo position,

Ndio maana toka Aje Arsenal hajawahi kucheza hizo nafas, japo tunajua akiwa kinda alipita hizzo nafas ,

Arteta kamsajiri kama AM, huku Smith Rowe nae Ni AM ,LW na false 9,

But Ni Rowe tu ndiye anaye rotate kwenye hizo nafas huku Odegaard akibak kama AM ,

 
kwa namna arsenal inavocheza hasa timu ikiwa n mpira ,odegaard role yake ipo clear kabisa kwamba ni playmaker ama kwa jina jingne AM na so far ameonesha kuimudu kwa kiasi cha kuridhisha nafasi yake..
 
Mwalimu pia amewataka lokonga, tavares, runnarsson...
Huu si uzi wa washabiki? Nia ya swali langu ni kujua mawazo ya watu kwamba hawa majamaa watatusaidia vipi, mfano abraham ni mrefu atasaidia kuokoa kona na kusimama kwenye ukuta kwenye freekicks
Anayemtaka ni mwalimu na anamkubali
 
Me sijaandika hayo kuhusu wewe kwenye issue ya Jesus au Tommy, bali ni overview ya mada kadhaa katika kipindi cha karibuni

Kwa upande wangu mie nasubiri Tu atakaekuja maana hakuna shabiki ambae hataki team yake iwe na striker/wachezaji Bora, ila sio kila club inaweza kufanikisha hilo na kama linashindikana basi ni kufanya kilichopo kiwe na ufanisi mzuri

Leo hii Arsenal yupo nafasi ya 4, dhidi ya team yenye kina Kane, Ronaldo,Sancho, Bruno,son,pogba dhidi ya wachezaji wa Arsenal kama Martin,saka,Rowe,Martinel,laca

Kwahiyo kwenye mpira sio mara zote wachezaji/majina makubwa yanaweza kukupa guarantee ya mafanikio, Kwa Aina ile ya wachezaji waliopo pamoja na uchanga wao na wanachokizalisha naimani kocha anajua ni kipi aongeze au apunguze, tulipasuka hela nyingi Sana Kwa Pepe na alipotoka alikuwa kaprove ila hadi Leo hajazalisha tulichotegemea coz system imemkataa

Kulingana na position ya Arsenal ulaya Kwa sasa ni ngumu ku compete na vilabu vyenye ushawishi juu ya majina makubwa, kwahiyo Unapokosa kitu unachokitaka katika Maisha inabidi ukipende ulichonacho na hakuna namna ingine

Mie Acha niendelee kusoma mawazo ya wadau Mkuu, ila sidhani kama Jesus ana ubaya huo ambao mmekuwa mnausema, maana ata km ww ndo ungekuwa Nunez/Halaand/vlahovic and the alike, ungekubari kwenda Arsenal?

Me naamini Arsenal inayotengenezwa sasa ndio itakuja kuvuta badae hayo majina makubwa Kwa kutumia resources ambazo zinaonekana za kawaida Kwa sasa ila zenye matokeo chanya, maana uzuri anachokifanya Arteta kinaonekana
 
Abraham na Jesus me sivutiwi na uchezaji wao Bora amlete mmoja ampe muda na imani Nketiah atakuja kuwa striker mzuri sisi watu wenye jicho la mpira tusha mwona
 
Dadaki Yani umununue Abraham kwa mchuzi wote huo pale bundasliga Kuna striker wazuri Sana
 


Mimi naona nikuache ndugu yangu nimeandika kila ninachojua. Siku nyingine.
 
Mwalimu pia amewataka lokonga, tavares, runnarsson...
Huu si uzi wa washabiki? Nia ya swali langu ni kujua mawazo ya watu kwamba hawa majamaa watatusaidia vipi, mfano abraham ni mrefu atasaidia kuokoa kona na kusimama kwenye ukuta kwenye freekicks
Runnarson ilikuwa backup na aliyeshauri alikuwa mwalimu wa makipa,

Tavares Ni backup LB , mm sijaona ubaya wake kias hicho, Zaid anahitaji kukua na kubadilika angle kadhaa ,

Lokonga namuelewa sana huyo dogo, Ni potential , najua Kuna criticism nying juu yake , ila ukweli dogo Ni potential ila epl tu inahitaji nguvu, mbona alicheza na Partey karibu game 9 hatukufungwa ,

Juz na soton man of the match Ben foster , possession 80 kwa 20 ,Kiungo lokonga

Sema weng mnaangalia matokeo na kuwatupia mzigo baadhi,

Ninachojua Arsenal ya Sasa haisajiri tu, Kuna sifa mwalimu anakuwa anazo za anayemuhitaji ,
 
Sijasema Jesus mbovu. Nimeandika kitu kingine ila hoja zinajengwa kwenye kitu kingine.

One of us is wrong. Mimi nakuacha. Siku nyingine.
 
Abraham na Jesus me sivutiwi na uchezaji wao Bora amlete mmoja ampe muda na imani Nketiah atakuja kuwa striker mzuri sisi watu wenye jicho la mpira tusha mwona
Yaani Nketiah unamuona Bora?

Mm ndio maana napenda kusema tumuache Kocha, akisajirri akifel atarud sokon,
 
kwa hizi crosses za wachezaji wetu?
Ndugu yangu, mimi nimewajibia wanaosema Tammy ni mwamba watakuja kutuelewesha zaidi ya hoja dhaifu ya kocha kamtaka.

Ila hata hivyo Lokonga ni mchezaji potential sana. Akiendelezwa vizuri utakua unamuangalia Verrati au Locatelli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…