credit to
AMBANGILE
CAPTAIN LACA .! 🔥
✍Arsenal wamepiga comeback kikubwa sana dhidi ya Wolves , waliwa search kweli kweli kwa dakika nyingi sana uwanjani na hatimaye kupata zawadi yao
✍Arteta alitumia mfumo ule ule aliotumia mechi ya kwanza dhidi ya Wolves 4-2-3-1 lakini inayobadilika kuwa 4-3-3 wakiwa na mpira ambapo Granit Xhaka anasogea juu kidogo lakini sio katika mstari mmoja na Odegaard ( yani Xhaka anakuwa namba 8 wa chini = deeper 8 , huku Odegaard anakuwa namba 8 wa juu = advanced 8 ) nini nia yake ??
✍Kwasababu Wolves nao wanatumia mfumo ule ule wa 3-4-3 maana yake ndani katikati wana viungo wawili tu Neves na Moutinho kwahiyo watakuwa wanakabiliana na viungo watatu Partey Xhaka na Odegaard lakini kwasababu ya Xhaka kusogea juu maana yake Neves na Moutinho hawawezi kumfanyia Pressing Partey ambaye anakuwa " SPARE MAN " kwenye kiungo ( mchezaji wa ziada ) , inawasaidia Arsenal kutawala mpira
✍Kitu ambacho Bruno Lage alikuwa anatafuta ni kuwavizia Arsenal kwenye counter attacks kwa kuwasubiri fullbacks wawili kusogea juu ( Cedric na Tierney ) ili namba 10 wake wawili Hwang na Podence kushambulia space iliyoachwa wazi .
✍Hii mechi kwa muda mrefu ilikosa ufanisi mbele ya goli , Arsenal walitengeneza nafasi nyingi sana lakini walikosa ufanisi ( Lacazette , Odegaard, Martinelli na Saka ) huku Wolves ( Jimenez, Hwang na Neto ) walipata nafasi nzuri za kuweka kambani lakini walikosa ufanisi
NOTE
1: Combination ya Neves na Moutinho inampa Bruno Lage nafasi ya kumaliza nafasi 7 za juu kwa uwezo wao kutawala mechi
2: Martin Odegaard , anafanya mambo magumu kuwa rahisi na vipasi vyake vya hapa na hapa ambavyo huvitarajii
3: Super Sub Pepe , turn and finish , lakini pongezi pia kwa Nketiah
4: Arsenal wanaonekana Fresh, sharp , fast , pressing sana, hawakati tamaa ...hivi vitu wakiongeza tena na ukatili mbele ya goli wataleta shida katika mechi zilizobaki.
5: PISHA NJIA HAPO KWENYE NAFASI ZA WATU , TOFAUTI POINTI MOJA KUTOKA NAFASI YA 4 NA MICHEZO MIWILI MKONONI....
Kafungwa Wolves wananuna wengine 😀😀😀
Full Time : Arsenal 2-1 Wolves