Me kuna muda nashindwa kuwaelewa kabisa baadhi ya mashabiki wa Arsenal wanaosema Arteta amefeli na afukuzwe, ohhh hana jipya, ohhh hana uzoefu,ohh hana mbinu hivi serious unapima mafanikio ya Arteta kwenye kikosi kile?
Unaposema me ni mrefu maana yake umekaa na Mfupi and vice versa is true, kwahiyo mnaposema Arteta kafeli mnamringanisha na nani hasa? Ambae alikuepo arsenal na wale wachezaji au aina Ile ya wachezaji na akafanya vyema?
Ukisema Arteta aondoke eti kafeli kocha amabe Anatumia vijana kutoka academy na wachezaji wengine wa kununua wa kuunga unga ulitaka afanye vizuri Kwa kiwango kipi labda na ukisema hafai ye aondoke hebu naomba nitajiwe kocha ambae ataweza kufanya vizuri akiwa na aina ile ya wachezaji waliopo na mnipe sababu za yeye kufanya vizuri
Hebu angalia competitors wa Arsenal vile walivojizatiti kiuwekezaji uwanjani hadi kwenye management, alafu njoo uangalie arsenal yako hivi kweli huoni aibu kukaa unalia na mwanaume mwenzio afukuzwe kazi eti kafeli
Kama wewe shabiki wa Arsenal unalia lia kutwa na kocha kwahiyo mashabiki wa Manchester utd pamoja na wachezaji wale ambao teyari wameprove wao ni Bora nao wafanye nini? Au wao team yao ni nzuri?
Kama unasema Arteta amefeli vipi kuhusu Ole Gunnar Solskjær pale utd ye tuseme alifeli cubic? Alikosa nini pale utd? Vipi kuhusu Mourhinho pale utd alikosa nini au nayeye hana uzoefu? Vipi kuhusu Mourhinho pale Tottenham au uzoefu aliuacha Chelsea? Vipi kuhusu Nuno pale Tottenham? Vipi kuhusu Ranieli? Vipi kuhusu big Sam? Vipi kuhusu unai pale Arsenal?
Shabiki akililia Arsenal iachane na Arteta eti kafeli nashindwa kumuelewa kabisa, hivi unaongeleaje namna bodi ya Arsenal inavoendesha team yao? Tangu yupo Wenger kocha ambae ana Heshima kubwa pale Arsenal ila ikifika kipindi Cha usajili hadi unamuonea huruma Mzee wa watu maana mabosi wao wanajali faida Tu na sio furaha ya mashabiki
Man utd pamoja na kununua wachezaji wenye viwango ila mashabiki wanalia na bodi kwamba inawaangusha ila Cha ajabu mashabiki wa Arsenal wanalia na Arteta mwenye akina Martinel, Saka, Smith,Tomiyasu,Ramsdale ndio masupa star wa team ila hawalii na kina krionke...! kweli Dunia haijawahi kuishiwa maajabu aiseee
Me nitakuwa mtu wa mwisho kabisa kuamini kwamba Arteta amefeli pale Arsenal, mpeni wachezaji wa daraja juu ndio tumjaji vile team itacheza na kuangalia mafanikio lasivyo me naona mnaendeshwa na mihemko tu na sio facts
Arsenal wamehangaika na Dusan weeee karibia week 3 ila ndani ya siku 2 Tu juve wameingilia kati na dogo anaenda Juventus alafu humu mtu unakuta analia na Arteta unataka alete Mke wake ndio afunge magoli pale kama wachezaji anaowataka bodi inashindwa kumpatia, jamaa anafanya kazi Katika mazingira magumu na inambidi atumie tu rasirimari alizonazo