Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kuanzia dakika ya 50 hata mechi yenyewe sikuiona walikata umeme huku nilikuwa nasikiliza audio commentary FotMob. All in all ukweli tuuseme. Bado kuna big WIP hapo arsenal.
 
Kwa kifupi Arteta sio kocha,top four tushatoka kwa mpira huu hii team sijui imelogwa na nani
 
Bado sikubaliani nawe mkuu.

Ni game tu tumetolewa basi. Partey huyo hapo sasa hata hiyo next game hachezi
Sasa Partey asipocheza na mid ikipwaya ni kosa la nani?

Kutolewa kutaka. Una options kwanini usizitumie? First game you posed a threat with 4 2 3 1 leo unaenda na 4 1 4 1 huku DM Lokonga ambaye game ya ligi na Liva alifanya mistakes za goli.

So hapa tutafute mchawi nani wakati kila kitu kipo wazi? Edu na Arteta wameharibu timu na kutoa wachezaji bila kuleta wapya kwa wakati. Mechi za ligi zitaanza huku hakuna mchezaji amesajiliwa.
 
Ooyaaa arteta anahitaji miaka mi5 mingine ili awe na maujuz ya klop.....alhamic iliyopita niliwaambia hapa acheni dharau madogo nyie kwa Liverpool bado sana

All in all mmepunguza idadi ya magoli maana huwag tunawapigaga nne kuendelea so congrats

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Adjustments.jpg
 
Season yetu imeishia jana rasmi FA out ,Carabao Cup Out,hatuna European competition yoyote ile but bado hata haya makombe tumewaachia wanaoshiriki European competition, Top 4 ipo rehani kwa asilimia 100 kwanza Tottenham Hotspur katuzidi points na michezo tumemzidi aliyocheza bado Manchester United anatupumulia na records za Arsenal vs Big Six zinafahamika(Manchester United Chelsea Liverpool Tottenham ya Conte )hawa wote wanatusubiri sioni jipya kwa sasa,no usajili wowote up to now tuendelee kuangalia mpira sababu tunaupenda but Season yetu imeishia January rasmi tusubiri next season angalau tupate hata kushiriki uefa ndogo tuendelee na ule msemo wa kupeana matumaini kuwa Arsenal performance yake inaimarika mno hata tukifungwa wakati msimu huu no trophies na kupata points 3 au kuwin vs Big Six ni ndoto za Alinacha

Klopp kashaanza kumsifia Martinelli kwa nguvu zote sioni Saka Martinelli Smith Row Odeegard Ramsdale ndani ya misimu 2 kama watabakia Arsenal hii hii ya Arteta Edu and Kroenke kama sio wawili basi atabakia mmoja katika hao
 
Na huyu beki wangu Gabriel sijui ataanza lini kujiamini maana anatushambulia sana na back pass zake. Anafanya mpaka Ramsdale ashindwe kupata muda mzuri wa ku distribute mpira mwisho tunajikuta tumepoteza.
Nadhani Gabriel hawezi kutupa tunachohitaji, ni wazi William Saliba anachukua nafasi yake next season.
 
Sasa Partey asipocheza na mid ikipwaya ni kosa la nani?

Kutolewa kutaka. Una options kwanini usizitumie? First game you posed a threat with 4 2 3 1 leo unaenda na 4 1 4 1 huku DM Lokonga ambaye game ya ligi na Liva alifanya mistakes za goli.

So hapa tutafute mchawi nani wakati kila kitu kipo wazi? Edu na Arteta wameharibu timu na kutoa wachezaji bila kuleta wapya kwa wakati. Mechi za ligi zitaanza huku hakuna mchezaji amesajiliwa.
4141 hiyo ni 433 LCM - ESR, RCM- MØ, lone 6 Lokonga.

Ukisema 4231 hapo kwenye 2 angekaa nani na nani kama Partey hakuanza? au ulitaka aweke pivot ya Patino X Lokonga? au tunaulaumu tu ilimradi tumeamua kulaumu
 
Back
Top Bottom