Usajili Updates: Arsenal wamtaka Vlahovic kabla ya msimu wa kiangazi.
Dosan Vlahovic.
Huyu ndie new marksman wetu mtarajiwa.
Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic na huenda wakamtumia Lucas Torreira kuwa uwiano katika ada ya usajili.
Arsenal tayari wapo tayari kuondokana na mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang hivyo kuweka nafasi kwa Vlahovic ambae ana umri wa miaka 21.
Lakini taarifa kutoka kwa vyanzo vya habari kama gazzetta del sport cha Italia zinasema Arsenal wameweka mezani dau la kiasi kama Pauni 58.3m na wanataka kuzuia mchezaji huyo kwenda timu zingine kama Tottenham na Juventus ambao nao wameonyesha kumtaka mchezaji huyo mzaliwa wa Serbia.
Antonio Conte huenda akajaribu kumsajili mchezaji huyo mwezi Julai endapo Harry Kane atakwenda Manchester City.
Juventus wanataka kumuuza Matthijs de Ligt ili kuongeza fedha za kumsajili Vlahovic.
Arsenal tayari wameruhusu Ainsley Maitland- Niles kwenda Roma kwa mkopo na pia wapo tayari kusikiliza dau kwa wachezaji Pablo Mari na Calum Chambers huku Alexandre Lacazette na Eddie Nketia wakiwa tayari kuondoka mwezi Juni baada ya mikataba yao kumalizika ifikapo muda huo.
Lakini habari ingine kubwa ni kwa Arsenal kuhitaji huduma za mchezaji wa kiungo Phillipe Countinho ambae hajaweza kucheza mara kwa mara akiwa na timu yake ya Barcelona.
Msimu ulopita Coutinho alikwenda Bayern Munich kwa mkopo kisha kurudi Barcelona msimu huu wa 2021/22.
Wawakilishi wa Coutinho walisafiri kwenda London mwisho wa wiki ilopita kujadili suala la uhamisho wa mkopo wa Coutinho ambapo sauala la mpango yaani payment structure ndo kizingiti.
Hivyo wakuu, Arsenal imepania kuhakikisha inashikilia nafasi ya nne kwenye msimu wa ligi na ikiwezekana kusogea juu zaidi kwa kuwa na wachezaji muhimu kwa kuzingatia kwa wiki tatu hatutakuwa na Thomas Partey na Mohamed Elneny ambao wapo kucheza AFCON.
Hivyo "fingers crossed" Vlahovic na Coutinho waje Arsenal kuongeza nguvu itakuwa jambo la mbolea sana.
COYGs!!!