Wadau poleni Sana kwa matokeo ya Leo. Kimsingi sote tumeumia Sana kama wapenda mpira na mashabiki kindakindaki wa arsenal.. Tupeaneni pole Sana!.. Hata hivyo sote tunaona mwelekeo wa timu yetu ni chanya kabisa.. Pamoja na hayo sasa wamezuka mashabiki katika jukwaa hili ambao wameanzisha tabia mbaya ya kutukana watu hapa jukwaani. Kuna huyu shabiki aliyetangaza kwa dharau kubwa kuihama timu yetu na kuanza kushabikia timu mpya, hata hivyo amerejea akiwa na tabia mpya ya kutukana watu matusi ya nguoni na Yale ya lejaleja.. Pengine amekulia katika makuzi ya kutukana tukana watu na hivyo kwake ni kitu cha kawaida.. Amekuwa anabadili style ya matusi na ukubwa wa matusi.. Wote tumeshuhudia matusi yaliyomiminika hapa muda mfupi uliopita... Kimsingi hili jukwaa linanajisiwa kwa matusi ya nguoni yasiyo na staha.. Yaani mtu hawezi kumaliza siku nzima bila kuwambia wenzake kuwa Hawana akili au wana IQ ndogo, utasikia maneno kama msenge, unachokonolewa, nitakupigia machine n.k.. Binafsi ninakerwa sana na huyu mtu maana anawatukana wana Arsenal na yeye eti anajiita mwana arsenal. Hivi huyu mtu ni shabiki wa Arsenal kweli? Kama ni shabiki wa Arsenal kwa nini asiwatukane watani wetu au wapinzani wetu? Hivi kweli wanna arsenal wanamkera kuliko mashabiki wa Chelsea, liver, spurs nk. Niwasihi Sana wadau tuonyeshe ukomavu wetu kwa kuvumiliana, kupendana na kujadili Moira kwa amani...