Will Jr
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 5,077
- 7,420
Sure mzee, kwenye profile Maddison anazidiwa na ESR kwa last season, hivyo inaonekana kweli Arsenal wanacheza kamari na hiyo pesaMaddison hana ukali huo. Mimi binafsi naona Arsenal tunacheza kamari hapa ya kuwaridhisha mashabiki.
Arsenal ina shida na mtengeneza nafasi Maddison ana takwimu gani za kumfanya awe mtengeneza nafasi wa kumlilia? Na bahati mbaya sana mtengeneza nafasi kwa miaka hii wa kiingereza amekua Arnold, beki wa Liva, na Kane mshambuliaji.
Kwangu mimi huyu siyo mchezaji wa kuuzwa milioni 70 ila hapa ndiyo tunarudi palepale tunaposema "Ben White hana thamani ya milioni 50 ila Brighton wanaamini hiyo ndiyo thamani yake, Lukaku hana thamani ya milioni 150 ila inter wanaamini hiyo ndiyo thamani yake, Grealish hana thamani ya milioni 100 ila Villa wanaamini hiyo ndiyo thamani yake"
Arsenal ikipata winger mwenye speed, finnishing na skills hata za level ya Mahrez niamini mimi pengo la Maddison halitoonekana.
Ila waingereza wanampenda sababu ni wao pia ni wazi ataongeza depth na productivity acha aje.
