David Luiz anaondoka.
Ametaka mwenyewe kuondoka. Mwingine anayetakiwa kuondoka naona ni Willian.
Inter wanamfukuzia Partey.
Zidane ameiambia bodi anaamini Odegaard angekuepo kuna mechi angeshinda kirahisi. Watu wa karibu wa Odegaard wamesema jamaa anajisikia kubaki Arsenal kwa jinsi anavyothaminiwa na kocha, wachezaji wenzake mpaka mashabiki.
Mislitant anasema Mavropanos amemuambia kama Arsenal itamrudisha ila hawi regular ni bora abaki kwa mkopo wa mara nyingine au uhamisho wa kudumu.
Newcastle imeonyesha nia ya kubaki na Willock.
Guendouz amesema anarudi Arsenal na akigewa chansi atajitoa kwa nguvu zote.
Bernd Leno amekanusha madai ya kutaka kuondoka amesema bado ana furaha Arsenal na siyo peke yake. Wachezaji wote wana furaha Arsenal.
Mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Laca na Arsenal yanaendelea. Inasemekana kuna uwezekano Laca akaitaka jezi namba 10 ambayo mwanzo ilivaliwa na Ozil. Emile anaweza gewa namba 9 au 10, ila Emile hajafanya mazungumzo ya namba ya jezi bado.
Pia Arsenal iko tayari kusikiliza ofa zitakazokuja kwaajili ya Willock, Niles, Torreira, Bellerin, Guendouz na Mavropanos.
Taarifa kutoka Arsenal inasema hakuna wakala ambaye ameonyesha ni tatizo Arsenal kutokuepo michuano ya Ulaya. Taarifa hii inakuja huku kukiwa na taarifa ya Kroenke kuahidi usajili wa wachezaji wakubwa watatu.
Inasemekana Arsenal inamfukuzia Camavinga ambaye inajulikana ni shabiki wa Arsenal. Mwingine ni Bissouma.
Kesho nitawaletea fununu za walengwa 3.