Sielewi watu wanaokuja hapa na kuamua ya kwamba hii game kwa Arsenal ni finito. Turudi nyuma kidogo, msimu huu huu huko huko Europa tulianza na matokeo ya kushtua kama haya.
Rennes alitufunga 3:1 tukawa na goli 1 tu la away wakaja Emirates, kilichotokea mnakijua.
Tukakutana na Olympiacos. Msimu uliopita aliyetutoa mashindanoni ni Olympiacos tulimfunga 1:0 kwake akaja kutufunga 2:1 Emirates. Msimu huu ikawa ni kurevenge tukampiga first leg na second leg akatufunga 1:0 tukasonga mbele.
Tukakutana na Slavia. First leg tukatoka 1:1 second leg Slavia akaoga mvua safi ndiyo tumekutana na Villarreal.
Villarreal katufunga 2:1. Ni ukweli tumecheza mpira mbovu, refa alikua miyeyusho, kocha hajafanya management vizuri ila 2:1 siyo matokeo mabaya kama timu itakua serious.
Mimi nasema bado tuna nafasi ya kusonga mbele. Pepe kasema "Tukutane London" Arteta kasema "Bado tumo kwenye hii game" akaulizwa una uhakika mtapindua meza akajibu "WE ARE ARSENAL"
Wiki ijayo siyo mbali.