Hii mechi hata sielewi Wenger atafanyaje manake kufunga haiwezekani, kina Bendt, schamakh na Arshavin wamekuwa vibogoyo tu. Nahii ndo aibu, ina maana bila Nasri, Fab au Persie hatuwezi funga?
Kila mechi wanashindwa ku-connect na naona Wenger bado hajapata solution manake anaendelea kuwapanga same way. Ni wachezaji wawili ambao wana style moja na wote ni wazuri wakiwa kati. Sasa unampompeleka Ben pembeni hana uwezo wa kumlisha Chamack matokeo yake wote wanabakia kuruka ruka tu. Kingine hakuna mtu mwenye uwezo wa ku-hold mpira, kila mtu anapoteza poteza na pasi mbovu kitu ambacho kinasababisha kushindwa hata kufanya mashambulizi.
Gibbs naona anakuwa open mara nyingi lakini hamna mtu anayejaribu kupeleka mpira kwake kutanua uwanja , kila mtu analazimisha mpira kati pale ambapo jamaa wamejaa.