Saa tisa na nusu tutakua nyumbani kwa Burnley tukijaribu kutetea kusonga mbele kwetu, kwenye karatasi na takwimu siyo game rahisi kwa Arsenal ya sasa.
Burnley wanacheza 4 4 2 hii formation ilitumiwa na Southampton kututoa nje ya FA, next game kwenye ligi tulishinda ila sikumbuki kama tulipata clean sheet.
Ninachokumbuka ni kwamba kwa msimu huu imekua ngumu kwetu kupata clean sheet kila tukicheza na timu inayotumia 4 4 2. Burnley hwana kikosi kile kile cha game iliyopita ambayo tulishuhudia Leicester akisakamwa kulia, kushoto na katikati.
Vardy ni scorer ila timu ikiwa in trouble Vardy hana kingine cha kuofa so siku ile alionekana anakimbia tu bila lengo same na siku tunawafunga 3 kwa moja.
Kwa taarifa ya muda huu inawezekana Emile akawepo au asiwepo kutokana na majeraha ya game iliyopita. Zaidi ya huyo kuna kipa Runar ambaye majeruhi yake hayaumizi kichwa as kuna Ryan tayari.
Tukishinda hii game tunaenda kua nafasi ya tisa na kumsubiri Villa apoteze game ili asitutoe hapo kisha tutakua na kazi dhidi ya Spurs ili kugombea kwenda nafasi ya nane. So hii game ya leo ni muhimu kama next game dhidi ya Olympiacos hivyo nataraji Arteta atataka kumaliza biashara mapema hivyo sitarajii kuona baadhi ya wachezaji wakiwa nje kwa kulenga kuwalinda na majeraha.
Tukutane baadaye.