Tunaifuata game na city kinyonge kweli kweli. Suluhu ambayo tulitakiwa tushinde huku defense ikiwa hovyo.
Ni lini umewahi kuona Arsenal kagewa odds 6+? Betika wameipa Arsenal odds 6.50, Betpawa wametoa odds 6.00 kwa Arsenal. Hili kwangu ni jipya, tumetembelea sana odds za 2 na 4 ila kwa game ya kesho sasa ndiyo tunaenda kiunderdog zaidi.
De Bruyne kapona, majeruhi walionao ni Nathan Ake ambaye hata alivyocheza alionyesha bado ana mchango mdogo, kisha na Gundogan, recently Gundogan is on fire.
Juzi Auba alipata chances 2 moja alibaki yeye na kipa baada ya krosi ya Saka akatoa nje ya pili alitaka kumfinya beki ila beki akaunasa.
Gundogan aliupokea mpira mrefu wa Ederson akamtesa Sanchez, Sanchez chali kama gunia akascore easily.
So we know jeuri ya kukabidhiwa odds 6 imetoka wapi.
Muda huu naandika Livescore inaonyesha Arsenal ina 35% ya ushindi City 42% na draw ni 23%. Sofascore inaonyesha watu 4876 wanatabiri Arsenal kushinda, watu 9727 wanatabiri City kushinda na watu 2572 wametabiri draw.
Zile back passes za juzi zilitokana na benfica kupaki basi au siyo now City hawatapaki basi na hivi karibuni wamerudia 4 3 3 na wanatumia mid na attacking fullbacks kutafuta magoli unlike baadhi ya opponents tuliokutana nao.
City ni superior kimbinu na quality ya wachezaji kwa sasa ni fair tukienda kujilinda na tukawa na striker ambaye anaweza kutoboa katikati ya watu, hivyo kwangu mimi Elneny na Xhaka wakae kati, Auba awe LMF, Odegaard awe AM, Saka awe RMF na ST awe Lacazette.
Pablo Mari kapona, Rob Holding yupo, Gabriel yupo, duo ya Rob na Gabriel na Rob na Mari ilitugea clean sheet nyingi sana, Luiz asicheze as City ni wazuri kwa kujiangusha na ni tatizo kua na beki kama Luiz unapocheza na divers.
Bellerin amekua shit, advantage yake huyu jamaa ni spidi. Kwa Arsenal ndiye mchezaji mwenye spid kabla ya Saka juzi kugewa 96 kwenye pace na Tierney kuja. So unatarajia aweze kumtrack Sterling, ila Sterling ana pace kubwa, diver na skills za kumwaga so ni sawa kabisa kuhisi atamsumbua Bellerin. Na kwa recent form unaona wazi Bellerin kazi anayo.
Ila kama mbwai iwe mbwai, Cedric awe RB na Tierney awe LB. Kimahesabu Arsenal hatuna chance ila hapana, tuna chance nzuri tu, lolote litatokea tulishawadisappoint City so kesho haitakua mara ya kwanza.
Wa kuchungwa ni mawinga, na Debruyne kama akipangwa. Kesho ni kesho anapasuka mtu.