Arsenal (The Gunners) | Special Thread

RIP My Team ujanja ujanja unafikaga mwisho ,kwa sasa tusubiri tutiwe vidole na Chelsea hakuna namna,kocha ni yule yule,Wachezaji ni wale wale, board ni ile ile sasa hayo matokeo ya ushindi Vs Chelsea yatatokea wapi?labda Lampard atudharau,but akikaza goli 3 wanapata Emirates na hii ni given!jana Elneny,Ceballos,Niles ambao ndo main midfielders wetu wamecheza na wamezidiwa zidiwa na 4 wamezipokea hvyo kisingizio hamna

Nasubiri May 2021 kuona kama tutabakia EPL au ndio Championship (kuna mashabiki wenzangu mtaani hawaamini kama Arsenal hatushuki Daraja that's fuckin stupid mind,kulikuwa na Aston villa Newcastle Nottingham Leeds na wengine mpaka makombe ya champions league walibeba na zilikuwa Big team kama Arsenal na zikashuka Daraja, timu zinazoelekeaga kudrop matokeo yao huwa ni kama ya Arsenal kufungwa fungwa fungwa weee,Arsenal siku atakayoshinda mean kupata point 3 katika mechi ,ni siku hata shabiki kama ana mke au GF atafanya hata Tendo la ndoa kwa raha zote

Kwa sasa Arsenal inahitaji kocha mpya, hata hiyo January Arsenal itampata mchezaji gani wa kiwango cha dunia?yupi?tuliwatakaga Grealish, Maddison na timu zao zipo Ok, tusidanganyane hakuna cha January wala nini tunapeana moyo,Kocha aje mpya ambaye atakuja na mbinu kali za kutubakiza EPL then Next season tutafute players wengine sababu Arsenal nusu ya wachezaji au timu nzima lazima waondoke na January hakuna timu kubwa ambayo itaruhusu wachezaji wake wasepe kirahisi namna hiyo never
 
Hivi hii timu inaelekea wapi

Mbona sielewei


Hivi uongozi hawaoni hili kweli
 
Wamekimbia uzi wao bana
.
Ni muda mrefu huu uzi ulisha kimbiwa.
Mtu pekee aliekua mbishi kufa ni Caste hata hivyo na yeye kaja na gea mpya kua yuko Njombe sijui, na alipo hakuna network.

Nime wamisi masela wangu wengi, akina Dully Jr, AronArsenal, Pweza na wengine wengi, yote hii ni sababu ya vichapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…