Yaani huwa nikikumbuka miaka ile ambayo tulikuwa hata hatufanyi sajili za gharama na bado timu yetu ilikuwa ni tishio kwenye michuano tunayoshiriki, halafu nikilinganisha na kipindi hiki ambacho tunatumia pesa nyingi lakini bado timu yetu inafanya utopolo tu huwa naumia kweli...
Kwa miaka takribani saba kisingizio chetu cha kutochukua ubingwa ilikuwa ni deni la uwanja, lakini hilo la uwanja limeisha ila bado mambo ni Yale yale tu.
Tumejitahidi kubadilisha walimu ila tumeshindwa kurejesha kile tulichokipoteza miaka 10 iliyopita, binafsi yangu kwa mara ya mwisho kuiona Arsenal yenye uwezo wa kucheza na timu yoyote na ukategemea matokeo bila wasi wasi ni ile iliyomtoa AC Millan pale San siro.
Hivi unafahamu timu nyingi siku hizi zikicheza na Arsenal zinakuwa na confidence sana kuliko hata pale zinapocheza na timu kama City au Liverpool haijalishi hata kama timu hizi zina majeruhi kibao.
Nawaza tu hapa ni lini tutarudi na sisi