Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Tatizo humu watu walikua na mategemeo makubwa kuliko uhalisia, hii timu bado kiukweli. Tutamlaumu Arteta bure ila hatuna wachezaji wenye viwango vya EPL.
Arsenal haistahili kupata haya matokeo kwa hawa waliotupita hadi sasa Southampton Crystal Palace Everton Astin Villa kwa mchezaji mmoja mmoja tumewaacha mbali mpaka salary wanazolipwa hvyo hiki sio kisingizio at all Calvert lew na Auba?Iwobi na Wilian? Tatizo litakuwa ni kocha na sio wachezaji
 
Mkuu Tatizo Arsenal siyo Kocha,Tatizo la Arsenal ni usajili,Huyo anayejiita mmiliki Bwana Kroenke Hatoi pesa ya usajili na anachokifanya ni kuokota wachezaji waliomaliza mikataba eidha wapo Huru au kununua wachezaji wa bei ya kawaida na wasio na viwango!,HAPO HATA UKIMETA MLAIKA KUIFUNDISHA HIYO TIMU HAKUNA ATAKACHO FANYA
 
Kingine ambacho najiuliza miaka ya karibuni Wachezaji wakija Arsenal huwa wanaporomoka sana viwango sana David Luiz ,Lacazette ,Willian Pepe, Torreira hawa ni mfano walikuwa wana viwango vikubwa mno but kwa sasa ni flop players ukiachana na Auba na Gabriel ambaye hajamaliza msimu kaonyesha ana kitu tatizo litakuwa wapi?
 
Napingana na wewe mkuu. Hivi unajua pesa aliyo-authorize tajiri kumnunulia pepe ndio kiwango hicho hicho liverpool walichomnunulia VVD???

mpaka dakika ya 58 auba amegusa mpira mara moja tu ndani ya boksi la Leeds na hii ni kwa sababu mipira haimfikii, tajiri tunamlaumu kwa lipi hapa??

Tajiri ametumia pesa nyingi kumsajili William Saliba na Leo edu na jamaa yake wanatuaminisha Saliba hafai???

Hivi ni tajiri ndio amemwambia arteta amuache ozil ili willock aje acheze namba 10???

Kweli tunampenda Arteta ila muda utaongea
 
Mkuu naona unatema sana nyongo. Pole mkuu Sisi tumeshazoea, mimi nimekuwa sugu sasa maana naiangalia Arsenal huu ni zaidi ya mwaka wa 20 sasa na hakuna msimu hata mmoja nimekosa game zaidi ya 5 za arsenal.

Ongea kwa sauti ya chini mkuu maana wakija utaitwa msaliti
 
Hakika mkuu
 
Tatizo humu watu walikua na mategemeo makubwa kuliko uhalisia, hii timu bado kiukweli. Tutamlaumu Arteta bure ila hatuna wachezaji wenye viwango vya EPL.
Sasa kwani anaetakiwa ajue hatuna wachezaji wenye viwango ni nani?? Hivi si ni yeye ndio alitakiwa ajue hilo halafu atafute hao wachezaji??? Kwahiyo Castr Aliweza kujua tatizo letu ambalo yeye alishindwa kulijua??

Hivi kweli tulishindwa Jana kucheza 4-4-2 halafu mbele tumchezesha auba na laca?? Au ilikuwa tu lazima tumchezeshe willock????

Auba tutaanza kumtukana soon ngojeeni tu.
 
Hapa umesanda mkuu. Hebu lete takwimu tuache maneno mengi kumlaumu mmiliki kila kukicha.

Arsenal squad ni kikosi cha nne au cha tano kw ughali pale EPL.

1. Manchester city
2. Manchester United
3. Liverpool
4. Chelsea
5. Arsenal
6. Everton
7. Tottenham
8. Leicester
9. West ham
10. Newcastle

Haya sasa unataka tujifananishe na Leicester?? Spurs??
 
Lawama limuendee tu Arteta na watu wake kudaadek zao.

Eti wakatuambia Torreira haendani na mfumo!!!!!! Wtf.....
 
Lakini hao wachezaji aliwataka Ni Arteta mwenyewe Arteta ndio alimtaka Willian na sasa hiv anamtaka mzigo mwingine Jorginho ambaye hata number Hana pale Chelsea Sasa hiv
 
4-3-3 ni mfumo uliosababisha majanga jana. kiungo cha Xhaka, Ceballos na Willock kilikosa nguvu kabisa, hivyo kuruhusu wale wahuni watawale mchezo.Kwa arsenal mimi ni muumini 3-4-3. Inaelekea Arteta bado yupo kwenye try and error. Pepe aliingizwa kwenye mtengo wa kijinga kujigonganisha na yule mhuni lakini alitakiwa kujua consequence ya ujinga wake. Kwa kiasi kikubwa aliigharimu timu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…