Thomas akimuongelea Arteta:
"Alikua mtu muhimu sana, yeye na Edu walinipa mipango yao na nilivutiwa nayo. Kila mmoja yuko tayari kushinda kila taji linalokuja mbele yao. Nafikiri hayo ndo malengo ya kila mmoja hapa na ni malengo yangu pia.
Akiongelea kwa nini jezi yake mgongoni ni 'Thomas' na siyo 'Partey' :
"Nimeona kwamba kuna Partey wengi kila kona na hata mpiga picha aliponiuliza kwa nini nilimjibu kwamba watu wengi wananifahamu kama Thomas, hivyo niliona nitumie tu Thomas"
Niliifuatilia #Arsenal kwa muda mrefu. Tulipo kuwa wadogo tulikua tukiangalia mechi nyingi sana, walipo twaa ubingwa bila kupoteza mchezo mwaka 2004, walikua vizuri sana. Pale ndo ambapo waliingia kwenye mioyo ya watu wengi sana.
Thomas akiongelea alivyo jiunga na #Arsenal:
"Wakala wangu alinipigia akasema inatokea na nilifurahi sana, sikuweza kulala usiku ule nilijisikia vizuri sana. Nilikua na furaha. Siku fika hapa ata lakini mashabiki tayari walisha anza kupagawa wakitaka nijiunge hapa."
Thomas: "Hii ni klabu bora, ni moja ya klabu kubwa kabisa Ulaya na ni klabu inayo stahili kuwa na malengo makubwa na nafikiri hayo hayatokei kwa siku moja, tunatakiwa kujituma zaidi ili kuhakikisha tunarudi tulipotoka. Nataka kumfanya kila mmoja awe na furaha."
#coyg [emoji837] [emoji836]
Sent using
Jamii Forums mobile app