Matarajio yangu leo tutashinda ila itategemea kama tukipata goli la mapema mfano dakika 15 za mwanzo, mechi itakuwa open na hapo tunaweza shinda kwa magoli zaidi ya mawili, ila Scot Parker atawaandaa Fulham watakuja na game plan ya kujaribu kuzuia tusiwafunge katika dakika 30 za mwanzo na wakifanikiwa hivo basi tunaweza maliza mechi na ushindi finyu something like 0 -1 au 1-2 na magoli ya kuanzia 70 minutes.
Ni mechi ya derby kwa hio ni ngumu zaidi itategemea fitness level ya mabeki wetu wa kati, udhaifu wetu hasa leo uko katika mabeki wa kati sababu tunaowategemea wako nje na majeraha,Mustafi, Mari na Luiz, na tuliowanunua bado hawana muda wa kutosha kwenye ligi hii Saliba na Gabriel, so timu leo nategemea tutacheza 4-3-3 na watakaoanza nategemea itakuwa kipa Leno, back 4 ya Bellerin,Holding, Niles na Tierney. Midfield 3 ya Xhaka, Elneny na Willian, front 3 ya Pepe, Nketiah na Auba. Hii ni game ya mchana inahitaji energy na pumzi, kati ataanza Elneny sababu ya fitness yake na pumzi, nyuma nimemuweka Niles na sio Gabriel sababu hiohio na mbele Nketiah badala ya Laca sababu Fulham watakaa deep, so Eddie ana uwezo wa kutengeneza gap kwa Auba ku-exploit na muungaiko na movements baina ya Niles na Tierney utawalazimu Fulham kufanya forced errors. COYG!