NILICHOKIONA KWA ARTETA HADI SASA
Hadi Sasa ARTETA amejitahidi kuingiza vitu vipya
Amestick na mfumo mmoja 4-2-3-1 , Emery ilikuwa kila mechi anakuja na mfumo mpya ,hii ilileta shida sana kwa wachezaji kujiposition na kuelewana.
Kama atabadilika bas ataenda na 4-3-3 kutokana na mahitaji ya timu
Amemrudisha LT11 nafasi yake na Xhaka amerudi nafasi yake halisia , hili ni jukumu la mwalimu.
Mpira wa Spidi na pass za haraka haraka , na Ku dominate mchezo , umesaidia kupunguza makosa kwa defenders , Awali ilikuwa timu inafanyiwa Shambolic ya mashuti hadi 25 per game .
Anakaa na mchezaji mmoja mmoja kuangalia uwezekano wa kuwapandisha viwango vyao
Ameimarisha build up ya kuanzisha mashambulizi ,
ARTETA anahitaji kila timu inapofanya mashambulizi basi wawe watano ,
Hii itasaidia upatikanaji mkubwa wa mabao .
Swala la kumaliza mechi kwa spid ile ile inatakiwa lifanyiwe kazi, japo tumeliona kwenye mechi 2 ya man u na ya Chelsea , naweza kusema huenda ni kutokana na timu tulizokutana nazo , na wao wana quality za kureact .
Kwa bornamouth haikuwa hivo ,
Ngoja tuone kwa hawa middle table team je spidi itapungua kipind cha pili.
All in all tuzidi kumpa muda .