Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Duuuh naona Big Sam kafukuzwa rovers noma sana.Jamaa huwa anasaidia sana kwenye timu ndogo ndgo hizi kuziweka sawa i hope atapa timu soon.Wampe Westham untd.
Aende west ham ama wigan, kop ndio wamegangamara na kocha wao.
Ebanae mechi ya leo ni ya 40 kati ya fergie na wenger na record ni fergie 16, wenger 15 draw 9 masaa kama yamegoma kwenda vile.
 
Maeneo ambayo kutakuwa na shughuli nzito ndani ya uwanja.

Kukiwa kumesalia muda mchache mpira uanze hebu tuangalie mechi hii muhimu kwa timu zote ambazo zipo katika kutafuta kikombe maarufu duniani cha Premier League.

Ni mechi ambayo itatoa mwelekeo wa timu zote ambapo endapo Arsenal itashinda itakuwa ikiongoza kwa 4 points lakini 3 points kwa Manchester City. Manchester United endapo itashinda itakuwa mbele kwa 2 points na itahitaji kuifunga pia Chelsea ili iweze kuwa kwenye njia nzuri ya kuelekea kunyakua kombe.

Nani na Gael Clichy

Nani aliweza kumfunga tera mara nyingi Gael timu hizi zilipokutana mwezi Januari na Man U ikashinda 3-1. Clichy pia alikuwa hana kasi sana kwenda mbele na Nani alimsumbua sana. Arsenal ilipocheza na West Ham alikuwa mwepesi na alisaidia sana ushindi wa 1-0. Ila tena walipocheza na Blackburn halafu baadae na Sunderland, Clichy alikuwa responsible kwa magoli ya timu hizo ambapo alishindwa kuwadhibiti washambuliaji wa pembeni ambao walisababisha magoli.

Hali hii imefanya nafasi ya Gael Clichy kuwekewa alama ya kuuliza. Hivyo leo tena Clichy ana kazi kubwa ya kumdhibiti Nani.

Theo Walcott au Robin Van Persie na Patrice Evra.

Evra amekuwa aki-struggle kwenye stamina ingawa amejitahidi kucheza vizuri kwenye champions league na mechi zilizopita. Endapo Arshavin ataanza basi kutakuwa na shughuli nzito ya kutafuta kupiga cross nyingi kwa Chamakh au kujaribu kwenda mwenyewe golini. Theo Walcott akiingia kipindi cha pili anaweza kuendelea kumchosha sana Evra na ataweza kumkumbusha kwamba kuropoka maneno bila heshima si kuzuri.

Samir Nasri na Darren Fletcher

Hapa ndipo mpambano utakapokuwa Nasri akiwa in-form na Fletcher nae akiwa amepumzika vya kutosha. Kwa kuwa Paul Scholes amepungua kasi na stamina ambapo yeye alikuwa akiweza kwenda mbele na kurudi nyuma, Fletcher atakuwa akijaribu mbele ya back four ili kujaribu kupunguza kasi ya mchezo na mashambulizi yatakayokuwa yakipikwa na Samir Nasri.

Hapa ikiwa Fletcher ataamua kwenda na kukaa mbele na kuacha nafasi katikati basi Nasri atakuwa hatari na Arsenal itapata angalu magoli mawili, kwa sabau kasi ya Nasri itakuwa kubwa kuliko Paul Scholes.

Andrey Arshavin na Rafael da Silva

Hapa ni uzoefu dhidi ya mtoto mdogo na Rafael atakuwa kijaribu kwenda mbele lakini hii itasababisha Arshavin kupata nafasi ya kuisumbua ngome ya Man U. Halafu pia Rafael ana hasira za ghafla na hali hio inaweza kusababisha kupewa kadi kutoka kwa refa ambae leo ni Haward Webb.

Kwa hio hapo Arsenal wataona Rafael ni njia ya mpito na ukizingatia Rafael alipewa kadi nyekundu Man U walipocheza na Bayern Munich na kusababisha timu yake kutolewa kwenye champions league.

Nemanja Vidic na Marouane Chamakh

Katika mechi 22 alizocheza Chamakh amefunga magoli 10, lakini leo anakumbana na Vidic ambae amesaidia sana kuirekebisha ngome dhaifu ya Man U huku akisaidiana na Rio Ferdinand. Kwa hio battle itakuwa kati ya wachezaji hao warefu huku Chamakh akijaribu kumiliki mipira na kuigawa kwa Wilshere au Arshavin au pia kufunga mwenywe na Vidic hatakuwa amelala.

Hapo ikiwa Chamakh atapata vizuri na Samir Nasri basi magoli yatafungwa na Arsenal lakini pia Vidic na Ferdinand hawatakuwa wamelala.

Rooney na Laurent Koscielny

Coscielny bado yupo "shaky" na mchezo wake akicheza na Squillaci mara nyingi hutokea kugongana na kusbabisha kufungwa magoli ya kijinga. Colcielny alisababisha Arsenal kufungwa na Chelsea na Blackburn na mpaka sasa ana kadi mbili nyekundu. Rooney anaonekana kurudia hali yake ya kawaida ya kusababisha magoli ingawa hajafunga magoli sana msimu huu. Alicheza vizuri dhidi ya Blackburn walipoifunga 7-1 na dhidi ya Valencia pia alikosa magoli mengi ya wazi.

Hapo tunaona kwamba kasi ya Rooney na kutaka kuthibitisha kuwa bado yumo inaweza kusababisha Arsenal kufungwa kwa uzembe wa Colcielny na Rooney huonekana akiwa hai sana wanapocheza na watani wao wa jadi.

Mwisho kwangu mimi naona matokeo yatakuwa ni kati ya yafuatayo.

Arsenal 1 Man United 0

Man United 1 Arsenal 1

Arsenal 2 Man United 1

Man United 1 Arsenal 0

Ni mechi ngumu sana hii.
 
Man Utd: Van der Sar, Rafael Da Silva, Ferdinand, Vidic, Evra, Fletcher, Carrick, Anderson, Nani, Rooney, Park

Arsenal ambayo ilicheza na Aston Villa na Everton ukiondoa Fabianski ambae ni majeruhi ni kama ifuatayo:

Arsenal

Szczesny, Sagna, Squillaci, Koscielny, Clichy, Song, Rosicky, Wilshere, Nasri, Chamakh, Arshavin

Subs:

Fabianski, Fabregas, van Persie, Walcott, Denilson, Djourou, Bendtner
 
Mkuu Wenger tusisahau kwamba Thomas Rosicky ameshiriki sana kuisadia Arsenal kufikia hapo ilipo.
 
Chamakh ataongoza mashambulizi dhidi ya Arsenal na Rooney ataongoza mashambulizi ya Man U, ni mitindo ya Arsenal 4-2-3-1 na Man U 4-5-1.
 
I just want to see an entertaining football match. See you in HT. Go Gunners Go!
 
Nani ameanza matatizo na Haward Webb anatoa onyo kwa maneno tu kwanza kwa Gael Clichy.
 
Ni mechi ya kwanza kwa keeper Wojciech Szczesny kwenye Premier League na leo atacheza vizuri amepata uzoefu pale Watford kwenye ligi ya daraja la kwanza.
 
Ji Sung Park,Anderson, Rooney na Nani wanaonekana tishio.
 
naona Arsenal wanapiga kiatu si mchezo, boys prove themselves to be men.
 
Back
Top Bottom