Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Jamani hamjasikia tetesi tetesi za Unai kufukuzwa huko kwenye ma social media ya Ulaya?.. Yaani huyu kocha siku akifukuzwa nitaandaa sherehe ili kusherehekea mwisho wa karaha na mateso anayotupa. Yaani tuna kocha mkuda sijapata ona, yaani sijui kwa nini hapendi torreila axheze kwenye position yake ya DM!.. Always anamchezesha out of position na anamtoa dk za 70+, na kila akimtoa baada ya dk 10 tunakuwa yumeshafungwa,, sasa cjui kwa nini huyu jamaa hajifunzi. Bodi ya Arsenal inatakiwa wafanye maamuzi magumu mapema, wakiendelea kumvumilia huyu mpuuzi tutajikuta tupo nafasi ya 10+ siku chache zijazo!.
Haya mkuu tunayaongea kila siku, we usijipe presha wewe just relax tu, huyu jamaa hata wamvumilie vipi itafika muda atafukuzwa tu, uwezo wake ni mdogo hautomfikisha popote.
 
Ukweli mchungu ndugu, tunafungwa magoli mepesi sana. Pia mbinu za kocha kwenye kujilinda ni mbovu.
Haiwezekani ukubali kushambuliwa muda wote ikiwa huna wachezaji wenye uwezo wa kukaba.

Hii Arsenal hata ikitangulia goli tano zinaweza kurudishwa zote.
Goli la Ayew vs palace ,goli la Origi la tano vs liverpool, na goli la Raul vs Wolves leo ni magoli ya aina ileile yanafanana,
Magoli Yote yanatokana na mipira ya kross, watu katikati hawaruki kucheza mipira ya vichwa utadhani wapo peke yao pale, yeye kama kocha anadeal vipi na matatizo km hayo??

Sababu si hiyo tu, ila kwa Unai nimeona vitu vingi kila siku ni the same old story, vinajirudia utadhani hatuna kocha, unakuwa ni utoto, vitu vilevile kujirudia kila siku...Na ndio maana Evra anatuita "my babies" ...yupo sahihi kabisa na aliongea kwa uchungu sio kwamba kejeli.
 
Kama atakuwa benchi katika hii mechi tusitegemee chochote kipya
Mkuu ndio maana nasema atafukuzwa tu, hiyo mechi sioni tukishinda labda by chance.Leicester wenyewe wanajua wakitupiga wanajitengenezea mazingira mazuri ya kukaa top 4, Na huo uwezo wanao mkuu, tena na hivi wapo Home.
 
Nilikuwa tu naangalia statistics hapa kwa hisani ya #Mbweha#
Dakika 90 mmepiga mipira mitatu tu golini...
Screenshot_20191102-220812_All%20Goals.jpeg
 
Unai hawezi kukaa Arsenal miaka mitatu kwa matokeo haya mkuu, Na ikitokea hivyo naamia Charlton Athletic ya kina Darren Bent na mdogo wake yule sijui nani Bent...
Wenger kakaa miaka 23 na makombe matatu na mlishindwa kumtoa, hamna uwezo wa kumtoa huyu. Kumtoa kocha inahitaji hela ndefu mazee..mtapata tabu sanaaaaaa.
 
aise uchezaji wa arsenal ni ovyo kabisa hadi selection alizofanya ni ovyo kabisaa torreira na ozil hawakucheza their natural position. kwenye subs ndio kabisaa.shukuru granit xhaka hajacheza...
 
Wenger kakaa miaka 23 na makombe matatu na mlishindwa kumtoa, hamna uwezo wa kumtoa huyu. Kumtoa kocha inahitaji hela ndefu mazee..mtapata tabu sanaaaaaa.
Hujui mpira mzee ni bora ukae kimya, we ulitaka awe na mangapi? nenda na wewe tuone utatoka na mangapi.
 
Duuh! Mkuu punguza hasira
Inaboa sana viongozi hawajui kama Mashabiki hawamtaki kocha au wanapuuzia ?nafikiri Mashabiki wa London ni wapumbavu sana ingekuwa TZ next match hakuna shabiki ambaye angeenda uwanjani uwanja ungekuwa mtupu kabisa hatutakagi ujinga
 
Back
Top Bottom