Wenger ndio alikuwa ovyo mkuu, ni mara ngapi umesikia Arsenal ina bajeti ya million 200 za usajili na wala hakuna cha maana kitachofanyika kwenye usajili paka dirisha linafungwa,utaona anakwambia nina coquelin, nina Chamak,nina wellbeck sihitaji hizo nafasii.Kitu kingine alikuwa ana allocate pesa kwa wachezaji wa ovyo kuamini watachange in future.
Thomas lemar aliweka £92m maji yalipomfika shingoni kipindi Sanchez anataka kwenda City, je hizo pesa alizitoa wapi tena dirisha dogo??, yule mzee alifanya kusudi sana kuamini kwa kile alichokua anaamini ndio maana MOU alimwita Specialist of failure coz alikuwa anaamini kitu kinachomfelisha kila msimu, hio ndio ilikuwa shida ya mzee.
Kumbuka mzee alikuwa ni manager hivyo Transfer policy ilikuwa chini yake, hakukuwa na Raul wala Sven by that moment.
Ila ndio hivyo,Kumbuka Dimitr payet wenger hakutaka kumsajili ingawa alionesha mahaba ya wazi, Riyad Mahrez wote walikuwa tayari kuja pale...all in all Ngolo Kante before Chelsea move Wenger alisema ana-Xhaka ambaye ni bora kuliko Kante.
Mkuu unajua pesa ya Xhaka kuja Arsenal ilikuwa kubwa kuliko Kante kwenda Chelsea.Pia ukumbuke Kante na Mahrez walikuwa offered kwa Wenger toka wapo France, tena wote kwa pamoja kwa bei ndogo sana wote kuliko tuliyomsajili Guendouzi.
Wenger ni legend wetu hatuwezi msahau lakini matatizo yake ni ya kimsimamo zaidi. All in all, he is a very good coach.