Ishu ni kwamba timu haina mipango, yaani paka Tuanzebe achomeshe boko ndio tupate goli.yaani timu imetoa draw na manchester united ndani ya old traford bado inalaumiwa, kweli binadamu tumejaa lawama na hatuna shukrani
Umeongea fact tupu, na ndicho tunachowaambia wanaomtetea Emery,Ishu ni kwamba timu haina mipango, yaani paka Tuanzebe achomeshe boko ndio tupate goli.
Paka sasa hivi unaweza kunambia kwanini tunapata matokeo ya ovyoo na kwa kubahatisha, je ni kwamba hatuna wachezaji wakutupa matokeo ya uhakika?
Ni lini unai ameshinda hata 3-0 au 4-0 kwenye EPL akiwa Emirates, kitu ambacho ilikuwa kawaida sna kipindi cha AW tunapocheza na midtables japo tulikua na Average players kuliko hawa wa leo.
Leo tukicheza na leicester,Watford,Wolves inakua km fainal eti sisi ndo tunapigwa 3-0, 3-1,...AW alikuwa anapoteza mechi na midtables ndio sikatai, lakini haikuwa kwa wingi huo wa magoli na azidiwe hadi ball possession , never.
Sisi tulitaka kocha ajaye aanzie pale AW aliposhindwa, ila huyu naona anaturudisha nyuma tuanze kujifunza hadi ball possession tena, AW kwa timu hii angefanya poa mara kumi zaidi ya huyu anachokifanya.
Fukuza huyu leta Ten hag tuenjoy football.
nakazia[emoji419]PER TAYARI AMESHA REACT KUHUSU FALSAFA YA MPIRA KUVURUGWA
“I’ve presented it to Edu,” Mertesacker reveals to The Athletic. The Brazilian was appointed as Arsenal’s first ever technical director back in July, and has since sat down with Mertesacker to sketch out the blueprint for the ideal Arsenal player. “Just to give you a brief idea: we want to dominate possession but we want to win it back as soon as...
KWANINI PER KAENDA MOJA KWA MOJA KWA BWANA EDU?(DIRECTOR OF FOOTBALL)
Director of football' ni nani? Ana kazi gani ndani ya klabu? Ukimuuliza Michael Zorc swali hili, atabasamu kidogo kabla ya kulijibu. Hii ni kwa sababu amekua akiifanya kazi hii kwa miaka mingi. Anajua kila kitu kuihusu kazi hii. Huwa anatamani kazi yake ifahamike zaidi kwa watu wengi. Kama vile kazi ya kocha inavyofahamika.
Kwa miaka mingi, kocha amekua na majukumu ya kuhakikisha anakisimamia kikosi cha kwanza, akademi na vikosi vya vijana kama bosi. Anafundisha falsafa zake ambazo anaamini ni bora kwenye kupata ushindi. Anakua na kazi ya kusimamia uhamisho wa wachezaji. Kuuza na kununua.
Anasimamia vitengo vyote ndani ya klabu. Kuanzia kile cha kutafuta wachezaji vijana hadi kitengo cha madaktari. Kocha anakua na kazi ya kutengeneza na kusimamia mipango ya muda mrefu ya klabu. Ndio maana kocha hakutambulika kama kocha pekee. Alitambulika kama meneja wa klabu. Alikua na majukumu mengi.
Hopefully Edu, Per and Freddie get together and recommend to Josh the all important change that needs to be made.
Lakin wewe hapo OT juzi juzi ulikula 4-0Jana timu yenye defence mbovu inakutana na timu yenye forward butu, utategemea draw tu
Man U wazuri nyuma na katikati wamefanana kidogo na Arsenal ila mbele ni butu
Arsenal wazuri mbele, katikati wamefanana kidogo na Man U ila Nyuma ni bomu
Ndicho kilichofanya jana mpira uwe hovyo, boring na hakukuwa na burudani kabisa. Utadhani Stendi na Singida United ndizo zilikuwa zinacheza. No game plan nzuri, no ball control, no dribbling, long passes ambazo nyingi zilikuwa zinafail. Majirani msipojirekebisha mid-table ni yakwenu hata top six hakuna