Baada ya Benitez kutoka Liva, ikapata makocha wa hapa na pale mpaka ikatulia kwa Klopp. Man U baada ya Alex kutoka wakazurura hapa na pale na saa hii wameangukia kwa Ole ambaye naamini ataondoka soon.
Chelsea wanaenda na kurudi kwa Mourinho, safari hii wametua kwa Frank, binafsi naamini siyo kwa kupenda isipokua wamekosa established coach ambaye angekubali kufundisha klabu isiyosajili.
Arsenal tumeachana na Arsene kaja Emery naona ghafla tuna hamu ya kuipita ruti waliyopita wenzetu. Ajiri, Tema, Ajiri, Tema tena. Yaweza kua Emery hatoshi lakini hapo ni tumemuweka sahani moja na Man City, Liverpool (Nimetaja hizi timu mbili kwakua ndiyo zina uhakika wa kushinda zinapocheza na timu nyingine) lakini kati ya hizi timu kuna moja ilijengwa kwa uvumilivu, trial and error mpaka wakafika wanapopataka halafu nyingine imejengwa kwa pochi.
By the time hizi timu zinajijenga, kwa pochi na kwa uvumilivu, sisi hatukua popote katika hayo makundi 2. Pesa hatukutumia na vipaji tulikua tunaviuza, hatukutumia pesa kuleta wachezaji wakali na vilevile hatukua na timu iliyosukwa kwa muda mrefu. So saa hii Emery ana timu ambayo imefungua pochi kidogo na ina makinda, ninachoona anajaribu kuwork out nani ni nini katika kila nafasi. Xhaka kuchezeshwa namba siyo yake siyo tukio la kwanza duniani, Henry alivyochezeshwa kama striker na Arsene hakuanza kuscore ghafla, ilichukua muda mpaka akawa tunayemjua leo.
Mgano tunajua kua mtu unahitaji beki wa kulia na kushoto wanatakiwa kua na speed kuliko CB ila Chambers hana speed ingawa ni beki mzuri. Mimi ningekua kocha nikicheza na baadhi ya timu siwezi kumpanga Chambers awe beki wa pembeni ni nitamweka CB au DMF. Emery anashinda na hawa watu karibia kila siku ni anajua nani ni nini katika nafasi anayompa.
Ingekua Man U ndiyo inalalamika kuhusu matokeo ningeelewa sana, kwanini? Kwasababu wametumia pesa nyingi karibia na Man City waliyotumia wanalipa wachezaji mishahara mikubwa lakini bado timu yao siyo tishio.
Miki nasema Emery ni kocha tena mzuri tu. Arsene alikuja akitokea Japan, na hakuna aliyejua huko alipotoka alifanya nini and the man turned out to be a legend. Emery hata historia yake ipo ila kumvumilia ndiyo mtihani au siyo? Kisa? Hajui kikosi. Nakumbuka fainali na Chelsea ya Europa kikosi alichopanga ni kilekile mashabiki tulikililia, tukafa nne, na huyu Ozil anayeliliwa hapa yumo.
Tukaga tatu na Leicester, tukafa 2 - 1 na timu jina limenitoka. Mimi nikisema Laca na Auba waanze hua simaanishi tunashinda hua namaanisha na sisi tunakua na fighting chance. Nikisema Matteo miyeyusho simaanishi asipokuepo tutashinda ila namaanisha akiwepo anaua fighting chance kwa ukosefu wake wa stamina na control.
Naamini baadaye kidogo tukitoka kwa Emery tutaenda kwa Luiz. Luiz ni mkabia macho kama Mustafi, na msababishaji penati mzuri tu. Tukitoka hapo tutaenda kwa Pepe, hajascore mpaka leo wakati Nketiah mechi moja tu kascore, Saka kashascore, tusihesabie la penati.
Hoja yangu ni kua arsenal bado tunajijenga, matamanio yetu yakae kando kama kusajili hata Totenham kasajili lakini maisha yake wote tunayaona na Efl kashatolewa.
Tuache mihemko.
Umeongea Vitu vingi ambavyo umechanga ukweli na uongo ,ila lengo mama ni Kutetea Upumbavu wa emery
Unasema Xhaka kuchezeshwa DM ni swala la muda tu atakaa sawa kama Henry alivyotoka winger to CF?
Huu ni uongo uliotukuka wenye lengo la kutaka kudanganya watu kuwa Emery ni kocha sahihi.
Kwanini nasema hivo?unatakiwa ujue Wenger alikuwa ni kocha anayewajua wachezaji kuliko wao wanavyojifahamu ,ndio maana wengi aliwabadili namba na wakafanya vzr kama kina kolo toure,eboue , rvp ,
Emery hawajui wachezaji hata kidogo .
Xhaka msimu wa 3 huu anacheza DM alianza chin ya Wenger ,a kashindwa na kuna sababu maalumu alichezeshwa DM , Wenger anapoondoka aliacha ripoti ambayo Arsenal ilibid waingie sokon kuleta DM , Kwa £26m LT11
EMERY kaendeleza makosa Yale Yale kumchezesha Xhaka DM ,
Na ameikost team magoli mengi,ameikost back 4 sana ,
Wewe unasema atabadilika ,nikwamba tusubiri misimu mingapi?
Nadhan umeona Emery ni kocha wa aina gan asiyejua Wachezaji wake ,
Unazungumzia kuwa emery alipanga kikosi kizuri fainal ya Europa,
Ulifatilia kweli mech za mwisho kila siku alikuja na mfumo mpya ,
Hicho kikosi kizuri alipanga wapi? Ikiwa kila alipotumia washambuliaji wawili hatukufungwa na takwimu niliziweka humu,ila fainal alikuja na 3-4-2-1 mfumo ambao unafanya auba awe mpweke .
Na ndio maana Ozil alimwambia WEWE SIO KOCHA
Unataka timu usiwe inafukuza ,hivi unadhan Liverpool bila kumfukuza king ken,Rodger w angekuwa hapo walipo sasa?
Kocha walau angeonesha basi ana vision
Kocha hana falsafa yoyote ile
Leo hii nikikuuliza Arsenal inacheza falsafa gani huwez kunijibu na uhakika 100%
Wachezaji inasemekana Hawamuelewi
Juzi Chamber kakataa kufata maagizo yake
Mech na Astonvilla wachezaji waliamua kujitoa binafsi ,Baada ya half time timu limefungwa 1-0 na red card juu, Emery anawaambia WACHEZAJI wakazuie timu isifungwe mengi nyumban
Wachezaji w anarud wanashambulia timu inashinda 3-2
Leo unatuambia Emery ni kocha mzuri
Sifa za kocha mzuri nadhan huzifahamu
Dirisha hili Kapewa £140m
Bado timu haijulikan inacheza NINI.
Naomba niishie hapa nitakuja kukujibu mengine baadae