*Watford vs Arsenal*
Uwanja : *Vicaurage stadium*
Eneo: *London*
*London Derby nyingine n hii hapa*



vs
Mechi inayowakutanisha Watford na arsenal Leo n mechi ya EPL ambayo itapigwa nyumbani kwa Watford Leo jioni ....mechi hii inawakutanisha miamba ambayo inatokea jiji moja Na majirani wa vitongoji yaani vinca.. na colonel ambayo ni maeneo yaliyopakana pale London.
Watford wanaingia uwanjan Leo wakiwa wa mwisho kwenye msimamo wa ligi kutokana na mwendelezo wa matokeo mabaya waliyoanza nayo msimu huu....na ilo limepelekea kufukuzwa kwa kocha wao *javi Garcia* na nafas yake kuchukuliwa na aliyekuwa kocha wa Watford na espanyol anayejulikana kwa jina LA *Quique Sánchez Florenz* ambaye Leo anaingia kucheza mchezo wake wa kwanza na *Unai Emery* ndani ya EPL....
Maisha ya unai na florenz kule Spain yalikuwa sio mazuri sana kwa unai je Leo kipi kitatokea pale EPL???
Arsenal inasafiri kwenda ugenini ikiwa haina record nzuri sana kwa game za ugenini ila yote n kutokana na kikosi kinachokuwa kikipangwa na ubora wa wapinzani ndo maana haipati matokeo mazuri ukilinganisha yale yanayopatikana wakiwa Emirates.
Leo kwa Mara ya kwanza ndani ya msimu huu tunaweza kumuona *Maestro mesult oezil* uwanjani maana hana tatizo lolote na hajacheza mechi zote nne zilizopita.....
Arsenal itaundwa na kikosi ambacho huwa n ngumu kukitabiri pale kwenye kiungo na ushambuliaji ila naiman kubwa kuwaona pepe,Auba wakianza na MTU mwingine pembeni....kufuatia kukosekana kwa lacazete....upande wa beki n wale wale Niles, sead, luiz,sokratis.... Viungo taarifa zipo tofauti ila tutegemee kumwona Matteo akiwa ndani pia Leo na akisaidiana na caballos na wenzake.
Upande wa Watford wao hawana injury kubwa sana ila wanaweza kuikosa huduma ya striker wao *Troy Denney* ambaye yupo injury na pahala lake sasa anacheza *Daniel welbeck* ivyo tutegemee kuiona Watford katika sura yenye mabadiliko kidogo tu pale kwenye kiungo kutokana na ujio wa kocha mpya ila wachezaji wengine watacheza wale tuliowazoea kuwaona..... Kwann nmesema kiungo ?..... Apo nmesema kiungo kwa sababu ndo eneo kubwa ambalo kila kocha huwa analifanyia kaz likiwa LA kwanza maana ndo moyo wa team unapokuwa.
Arsenal imeshinda mechi tatu za mwisho ilizokutana na Watford.....
Watford hawajawai kupoteza mechi zao tatu za mwanzo za nyumbani toka 1992 ....
Arsenal imeadhibiwa penalty 9 toka msimu uliopita....
Watford wamepoteza mechi tano kwenye mechi zao sita za nyumbani walizokutana na arsenal.....
Kutokana na rekodi izo na ukiangalia ubora wa vikosi kila upande na mazingira ya mchezo n kwamba mechi itakuwa ngumu na yenye ushindani ila mwenye kuchanga karata vzur Leo ndo ataibuka mshindi.
Arsenal wana wachezaji ambao Leo wana ule uwezo nusu wa kuamua matokeo MTU mmoja na wanatakiwa wawe bora sana ...Watford pia wana hawa watu akina Pereira wanaweza kuumaliza mchezo muda wowote ivyo ubora wa pande zote mbili hasa mabeki wanatakiwa kucheza kwa umakini sana Leo.
Utabiri wangu kwa Leo naiona arsenal ikishinda mchezo huu.
Asante