Wataalam wanasema Mbwa ukimjua jina, hakusumbui. Ni kama vile mie, siumizwi na Arsenal yangu kwa sabbu nimeweza kuijua.
Lakini kuna kitu wengi hawajakijua au wanakijua hawajakipuuza. Wengi sana wanaamini Arsenal tatzo ni Stan Kroenkee, . Nimewahi kuandika makala kuhusu huyu mtu, sitaki kurudia sana.
Ukichimba sana, Kroenkee si kua ni tatzo pekee au tatizo kubwa. Tatizo kubwa ni wanaoendesha masuala ya kimichezo. Sabbu klabu ni kama kampuni. Kampuni hua inauza product, product pale Arsenal ni mpira. Sasa walio ktk uzalishaji ndiyo wana matatzo zaidi.
Stan ni bingwa wa uwekezaji ktk michezo,na yeye hutumia self sustainability model ( kwamba klabu ijiendeshe yenyewe), sabbu yeye ni enterprenuer (mjasiria mali), siyo mwekezaji. Sasa wengi hudhani Stan hua anachukua pesa zinazozalishwa na Arsenal. Yeye alinunua hisa za pound milion 700+, mwaka 2011, akawa na 67% , na 2018 ametoa ofa ya milion 600, kwa hzo 30%. Total bilion 1.3. Thamani ya Arsenal kwa sasa ni 2 bilion. Kwahyo Stan yeye faida, ataipata kama akija kuamua kuuza hisa zake zote. Lets say Akiuza bilion 3 mwaka 2022, faida itakua ni hiyo , siyo pesa za makombe au viingilio.
Sasa yeye haweki hela Arsenal sabbu aliwaachia wao wazalishe, walipe matumizi yote, zinazobaki wasajili, yeye hagusi chochote ktk hizo pesa. Ndiyo maana klabu inajiendesha yenyewe. Liverpool wanafanya hivi, United wanafanya hivi, na model za kimarekani zipo hivi. Sabbu wao hawangaalii zaidi makombe, halafu klabu ina madeni au pesa zitoke mfukoni, klabu haizalishi.
Tatizo kubwa Arsenal ile Era iliyoisha ya Wenger na wenzie, ni zile wakiachiwa wanawekeza vipi? tuchanganue. Arsenal ilikua inanunua wachezaji wengi wanaocheza nafasi 1, Wilshere, Carzola, Ramsey, Oezil wote no 10, Rosicky, Arshavin, Nasri. Na mara nyingi walikua hawatatui matatizo, shida no 6, analetwa no 10, shida striker analetwa no 7, shida beki wa kati, analetwa no 10. Mfano kulikua na haja gani ya kununua Auba na Laca ndani ya mwaka mmoja wakati wote no 1?, na Giroud alikuwepo?
Pia walishindwa kukubali kua ile british core, ilishindwa na kuwaondoa mapema. AOC, JERKINSON, WILSHERE, RAMSEY, WALLCOT, hii project ilifeli, na walikua wakilipwa mishahara mikubwa kuliko uwezo wao. Sasa hata ile pesa iliyokua inaachwa na Kroenkee haitumiki vzuri. Arsenal ina Wage bill nzuri ni ya 9 kw Ulaya Nzima, pound milion 245, wanatumia, ndiyo maana unaposema Kroenkee hatoi hela anakushangaeni. Kila klabu ina budget yake, hawawez kufanya vile ka Psg. Hizo hizo watumie vzuri.