Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Vijana wameahid ushindi kesho

Naiman manyua hawatatuangusha katika kuwabonda Chelsea,

Maana akifungwa kesho matumain yake kuingia top four yanabak 1% ,

Screenshot_2019-04-27-23-28-09.jpeg
 
Mimi naamini kwenye mfumo wa kukuza vipaji na Ajax Amsterdam wamedhihirisha hivyo.

Tusije kushangaa kuona Ajax wananyakua kombe la CL.

Arsenal na Emery wana haki ya kukuza vipaji na kuviendeleza na wakati huohuo wakisajili wachezaji wazoefu ili kutafuta timu imara na yenye uchu wa ushindi.

Arsene Wenger alikuwa ni mmoja wa makocha bora sana lakini alikosa kitu kimoja kikubwa kwenye suala la usajili kwamba nae alihitaji kusajili kwa akili.

Alikosa hivyo, na alipokuja mkurugenzi wa mpira bwana Sven Mislintat ndiye aliewasajili Matteo Guendouzi na Lucas Torreira ambao wamekuja kuwa baadhi ya wachezaji nyota wa Arsenal msimu huu.

Tusisahau pia kwamba kila timu ina mfumo wake wa biashara au Business Model na unaendeshwa vipi.

Pale Manchester City, mwarabu anaingiza pesa zake kutoka mfukoni na mara nyingi tu wamevunja sheria za matumizi ya fedha za ziada ya "financial play rule'' mara nyingi tu na ni wachezaji wangapi wameuzwa kutoka man City kwenda timu zingine zaidi ya kusajili wachezaji zaidi?

Na sasa hivi Manchester City wanapanga kumsajili mchezaji wa kiungo mkabaji kuja kuziba pengo la Fernandinho aitwae Rodri kutoka Athletico Madrid ambae akagharimu kiasi cha Euro milioni 58!

Fernandinho mwaka huu mwezi Mei atatimiza umri wa miaka 34 na ameanza kuchoka.

Hivyo Manchester City wao wanacheza kihuni kwenye "transfer activities" kwa mfano walitoa pesa mfukoni pauni milioni 60 na wakamsajili Mahrez ili kumzuia asiende Arsenal msimu wa 2017/18.

Sasa hivi Mahrez analalamika kukosa kucheza wanafikiria kumuuza tena lakini watasema asiende kwenye timu pinzani.

Pia pale Manchester City yupo Danilo ambae Manchester City walimsajili kwa pauni milioni 26.5 msimu wa 2017/18 ambae mpaka leo anasugua bench.

Liverpool waliwauza Suarez kwa Barcelona kwa pauni milioni 75 hivi, baadae wakamuuza Phillipe Coutinho pia kwa Barceona kwa pauni milioni 142.

Sasa Liverpool wametumia vizuri pesa waloipata wakasajili wachezaji kama Sadio Mane kutoka Southampton (pauni milioni 34), Mohamed Salah (pauni milioni 36.9) kutoka Roma na baadae wakamsajili beki wao mshahara Virjil Van Dijk kwa pauni milioni 75.

Manchester United wao wakaingizwa mkenge na tapeli wa Ureno Jose Mourinho na tumeshuhudia jinsi walivyotumia kiasi cha pauni milioni 400 kwa wachezaji wapatao 11.

Manchester United wamemlipa tapeli huyo Jose Mourinho pauni milioni 18 kutokana na kuvunja mkataba nae.

Tottenham wao hawakusajili hata mchezaji mmoja katika msimu huu (khasa mwezi January) kwasababu wao wametumia zaidi ya pauni bilioni 1 kujenga uwanja wao pale White Hart Lane na hakuna mtu ambae amepiga kelele kama walizopigiwa Arsenal walipojenga uwanja wao pale Ashburton Grove.

Hivyo kila timu ina mfumo wake wa biashara business model na matumizi ya fedha wanazopata iwe mikopo au fedha za kutoka kwenye akiba benki zinazotokana na mauzo ya tiketi, nguo na vifaa vya michezo au merchandise na vyanzo vingine.

Tujifunze pia kutoka kwenye timu kama Watford na Wolverhampton ambazo zaendeshwa kwa bajeti ndogo lakini kuna matokeo makubwa sana uwanjani.
Ujue wengi mpira wameujulia baada ya kubeti kuja,

Kuna mwingine anaweza kudhan Liverpool ni wamwagaji wa hela kumbe hapana ,ni hela ziliwatembelea baada ya mauzo ya Suarez na cou 10, wakazitumia vzr wamejenga timu,

Na sasa hivi wamesema hawataspend sana ,means labda utokee mzigo tena wa maana,
Ninachotaka kusema unaweza kuwa na hela kidogo ukaspend wisely,

Hivi unaweza kujiuliza kulikuwa na haja gan ya mou kujifanya anajua kutoa 52 kwa Fred wakati kulikuwepo kina filipe Anderson WA 35,

Utaona ili timu isiwe inaingia mkenge kila Mara anahitajika MTU au watu WA mpira nyuma, hiki kitu city wamekifanya,

Na arsenal tumeanza mwaka Jana ,

Ndio maana Barcelona walipotaka tutoe 20 kwa Denis Suarez, watu WA mpira wakasema hapana , tunamuomba kwa mkopo, then tutaangalia mwisho WA msimu, tulipe hiyo 20 au tumrudishe,

Lakin kama una watu wanaospend ovyo, ndio yanatokea Yale Yale yakina bakayoko, elneny, Fred
 
Unai Emery: “In the Premier League, technical quality without physicality is not enough. City, Liverpool, Tottenham, Chelsea, all the top teams here are physical and technical. Arsenal need to be the same.”


Kitu ambacho watu pia hatujakifahamu
 
MAKOSA YALIYOTUGHARIMU MECHI MBILI MFULULIZO

NI KUKOSEKANA KWA VIUNGO KATIKATI, MECHI YA WOLVES EMERY AKAFANYA MAKOSA TENA AKAJA NA 4-2-3-1 HUKU NAMBA 2 NILES AKIWA BADO HAJATENGEMAA, NAMBA 3 NACHO KASI IMEPUNGUA, AKAMUWEKA BENCH KOLASINAC AMBAYE AMEKUWA AKICHEZA VZR NA IWOBI UPANDE WA KUSHOTO


KUELEKEA MECH YA LEO

KAMA LEO TUTARUDI KWENYE MFUMO AMBAO TAYARI WACHEZAJI WAMESHA UADAPT WA 3-4-1-2

BASI NI DHAHIRI TUTAREJEA KWENYE NJIA YA USHINDI ,

HIKI NDIO KIKOSI AMBACHO KUFUNGWA HUWA NI MWIKO

NAIMAN KUREJEA KWA AUBA, KOLASINAC

KUTAFANYA TUANZE NA 3-4-1-2

PALE MBELE TUKIANZA NA DOUBLE STRAIKERS , NYUMA AKICHEZA OZIL

USHINDI LEO NIMUHIMU HUKU TUKIOMBEA NJAA CHELSEA APOTEZE AU SARE ITAPENDEZA ZAIDI.

COYG
arsenalsection-20190428-0001.jpeg
 
Jitambulishe ,wewe ni nan na unatokea timu gan tujue ni cheltako, nyumbu au n.k
Unai Emery: “In the Premier League, technical quality without physicality is not enough. City, Liverpool, Tottenham, Chelsea, all the top teams here are physical and technical. Arsenal need to be the same.”


Kitu ambacho watu pia hatujakifahamu
Icho kitu mkuu mi nimekiona muda sana, timu yetu wanalegea sana tunapokua away frm home, sijui hata kwanini... waga km tunataka mambo yajiset yenyewe,
 
My predicted lineup for tomorrow’s game away at Leicester
Overall I think we will go back to 5 at the back, as we played a back 4 against Wolves & we played terribly.
Aubameyang is back from his injury that prevented him from playing on Wednesday, so I think he will start alongside Laca tomorrow.
Comment below who you think will play.
COYG
View attachment 1082908
bado unaendelea kuliamini hilo tambara hapo golini
 
Mechi ya leo mashabiki wenzangu wa Arsenal naona hatuna nayo mzuka kabisa yaani baada ya kufungwa mechi 2 mfululizo na hasa ya Crystal palace hata Mimi mpaka sasa sielewi itakuwaje top 4 sitaki kujipa matumaini nkaishia kuumia moyo
 
Back
Top Bottom