Msiwe na wasiwasi, Arsenal watashinda mechi ya marudiano kwenye uwanja wa Emirates.
Mechi ya jana ilichezwa kwenye joto la chini ya nyuzi 0 kwenye baridi kali hivyo kwa kiasi fulani kuliathiri uchezaji wenye ufanisi.
Halafu msisahau Lacazette alifunga goli na likakataliwa kwa sababu ya kuwa offside.
Isitoshe kuna wiki nzima ya kujiandaa kuja kuwashughulikia hawa watengeneza matrekta Alhamisi ijayo.
Ila hawa jamaa walijiandaa kwa kuwa na likizo ya baridi (winter break) kwa wiki tisa mfululizo hivy kuipa mechi ya Arsenal umuhimu wake.
Pia kama mnamkumbuka Alexandre Hleb nae alikuwa ni mmoja wa wachezaji wa kiungo wa timu hii huku akiwahamasisha wachezaji wadogo kwake kucheza kwa bidii (Hleb ana miaka 37 sasa).
Alex Hleb amehirisha kabisa kustaafu kucheza soka mpaka acheze na Arsenal mechi zote mbili nyumbani na ugenini, hivyo utaona jinsi hawa jamaa walivyojiandaa.
View attachment 1022896
Nacho Monreal, Alexandre Lacazette na Saed Kilasinac wakiwa wamevaa sweta za mikononi (Gloves) kutokana na baridi kali la nyuzi chini ya 0 mjini Barisaw nchini Belarus.