KWA NINI ARSENAL HAWAKUSAJILI JANUARY, WATASAJILI DIRISHA LIJALO? MWELEKEO WA TIMU NI UPI?
mashabiki wengi wa Arsenal hulalamika bila kutumia muda wao kufuatilia mambo yanayoendelea kwenye timu yao
Dirisha la January ...
Kuna sheria ya financial fair play ambayo ni ngumu kueleza lkn kwa ufupi inakutaka kutumia kulingana na mapato yako. Mfano huwezi kukopa kwenda kununua mchezaji. Sheria hiyo pia inasema matumizi ya mshahara yasipande kwa zaidi ya asilimia 7 kwa mwaka. Arsenal walikamatwa na kifungu hiki.
Wachezaji waliosajiliwa karibuni na mkataba mpya wa Ozil Unafanya kiwango cha mishahara Arsenal kufika kikomo. Ozil anapokea paundi 350000 kwa wiki, Auba 200, Miki 170, Laca 150, Sokraits 90. Kumbuka timu haiko Champions League msimu wa pili. Ndiyo maana waliwafuata Suarez, Perisic, Carrasco na Nkunku wachezaji ambao wangepatikana kwa mkopo ili signing fees zao zigeuzwe mshahara
Dili karibu zote zilishindikana kwa sababu vilabu viliwataka Arsenal waji commit kwamba watawanunua mwisho wa msimu. Arsenal walikataa kwa kuhisi wanaweza kuji commit alafu mchezaji asifikie viwango walivyotarajia.
Watanunua dirisha lijalo?
Mtu atajiuliza kama ni hivyo wataingia sokoni dirisha lijalo? Ndiyo kwa sababu 2, kwanza kuna wachezaji wataondoka na hivyo kupunguza mzigo wa mshahara. Chech paundi 100000, Ramsey 1000000, Mustafi 100000, Welbak 85, Jenkson 65 na kuna uwezekano mkubwa Ozil 350 na Nacho 100
Pili ni ufadhiri wa Adidas, Emirates na serikali ya Rwanda ambao mikataba yao inaanza July 1 mwaka huu. Hapa naomba ieleweke siyo kwamba Arsenal hawana fedha bali mapato haya mapya yanaruhusu kufanya matumizi makubwa na hasa kuongeza mishahara. Watu walio karibu na klabu wanasema watakuwa na karibia paundi mil 100 kabla ya mauzo. Ingawa itategemea pia kama watakuwa Champions League. Defender, Winger na beki tatu ni vipaumbele.
Na Aroon ze gunaz
Sent using
Jamii Forums mobile app