GUENDOUZI WA ARSENAL ANANICHEFUA-BERBATOV
Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham na Manchester United Dimitar Berbatov amesema kinda wa Arsenal Matteo Guendouzi anacheza vizuri mpaka inafika mahala anamkera kwa ubora wa kiwango chake.
Guendouzi mwenye miaka 19 amekua akicheza kwa kiwango kizuri tangu asajiliwe na Arsenal kwenye majira ya joto kwa ada ya paundi milion 7 tu (milioni 200 za kibongo). Akiongea na kituo cha SkySports Berbatov alisema
Uyu dogo ana miaka 19, lakini anavyocheza utadhani alizaliwa akicheza Uingereza, anacheza kama alikua hapa akicheza miaka mingi iliyopita.
Wakati mwingine natamani ningekuepo uwanjani ili nipambane nae kwa maana ananichefua kwa namna anavyojiamini uwanjani.
Anajiamini sana akiwa na mpira na yupo kila mahali uwanjani. Katikati utamkuta,pembeni,nyuma,mbele yupo kila mahali.
Unaweza ukawa na miaka 19 lakini ukawa na moyo na hulka kama ya mtu mwenye 24, haijalishi una umri gani linapokuja swala la kuonesha ubora kwenye mpira. Ndivyo alivyo Guendouzi.
Matteo Guendouzi ameichezea Arsenal mechi 13 katika mechi 16 za ligi kuu ya Uingereza. Kiwango chake bora kimewafanya wachezaji kama Mohamed Elneny na Aaron Ramsey kukaa benchi. Kama akipata malezi mazuri anaweza kua moja mmoja wa viungo bora ulaya kwa miaka inayokuja.
Kuna mshabiki mmoja wa Arsenal niko nae hapa. Sijui ni mlevi, anasema Matteo Guendouzi ni mzuri kuliko Michael Carrick.