Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Lakini Bado ipo Mbele ya Arsenal Kwenye Ligi na kwenye Kila Kitu 😀 😀 😀
Hongera mkuu kwa ushindi wa leo......waafrika wameing'arisha liver leo naona kicheko tu.......mo salah....s mane tchao
 
Before WWI
 
FT
Östersunds 0-3 Arsenal
Hawa jamaa niliwacheki kwenye pre-match meeting walikua wanataka Arsenal waweke kikosi chao kamili ili na wao wajipime ubora wao.
 
Nadhani pale golini, Wenger afikirie kumwanzisha David Ospina badala ya Petr Cech ambaye anaonekana amechoka siku za hivi karibuni.
 
" Nitamaliza mkataba wangu"

Arsene Wenger amesema kwamba atamalizia mkataba wake uliobaki wa mwaka mmoja na nusu ndani ya Arsenal baada ya kuibuka kwa uvumi kwamba ataondoka Emirates mwishoni mwa msimu huu.

Wenger mwenye umri wa miaka 68 alisaini mkataba wa miaka miwili mwishoni mwa msimu uliopita , lakini kukiwa na wasiwasi wa Gunners kukosa kuingia ndani ya nne bora kwa msimu wa pili mfululizo , kumekuwa na taarifa kwamba Wenger huenda akaondoka mapema.

Hata hivyo Wenger amekanusha taarifa hizo , akiiambia beIN Sports:

" Siku zote nimekuwa nikiheshimu mikataba yangu, ningependa kuwakumbusha, nilisema hapana kwa vilabu vyote vikubwa Duniani kwasababu ya kuheshimu mikataba yangu, kwahiyo hiyo ndio najaribu kufanya mara zote."

"Baada ya hapo, pia inabidi tukubali katika kazi zetu , kwamba maisha ya baadae ni maisha ya baadae tu, lakini kwangu mimi, maisha ya baadae ni kushinda mechi ijayo."

" Inabidi tucheze vizuri katika kila mechi na kuonyesha mpaka mwisho wa msimu njaa ya kushinda kila mechi . Hicho ndio kila kitu kuhusu sisi."
 
Mkuu wakumbushe pia week end hii kuna mechi za FA, na mpaka sasa Lukaku 2 Huddesfield 0.
 
Arsenal na Emirates wametangaza ku-extend mkataba wao wa udhamini so far wamesema ni record breaking,tusubiri tusikie yaliyomo.
 
Hivi mmeona wanaume tunavyo cheza.? Hata kama una kikosi kibovu isiwe sababu mtu kukunyanyasa. Tumia ulichonacho vizuri kitakufaidisha. Siyo mnakaa kaa kizembe.

Sema one day na nyie mtakua kama sisi. Hiyo stage na sisi tulipitia. Ila muwe mnakuja kuangalia kaka zenu tunafanya nini. Msikae kizembezembe tu.


Mje weekend muone tutakacho mfanya Man U kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…