Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mkuu achana nae huyo ni mke wangu yupo mp Siku ya pili leo.
Hahahaha watu mnautani wa ngumi au anahis tutakuwa moto kwa hizi ngoma nne Ozil, Micky, Auba na Lacazett huku kati yupo Jack na Xhaka sipati picha ngoja tuone inakuaje
 
Bado tuko na kizungu zungu tokana ngeu 3 za jana, manundu yanatuuma mno..kama kawaida yake AW, anajifanya kuyapoza na P Aubemayang...Ila Cech wakuu keshazeeka, tukubali tukatae, kila kizuri kina mwisho wake, time for Ospina between the posts, NOW!..Ila babu atafanya hivyo?!
 
Ni rasmi Pierre-Emerick [HASHTAG]#Aubameyang[/HASHTAG] sasa ni mchezaji wa Arsenal, klabu hiyo ya London kaskazini imetangaza.
Aubameyang ametia saini mkataba wa "muda mrefu kwa uhamisho ambao umevunja rekodi ya klabu" kutoka Borrussia Dortmund.
"Mchezaji wetu wa pili wetu kumnunua wakati wa kipindi cha kuhama wachezaji Januari. Auba ni miongoni mwa washambuliaji stadi zaidi duniani. Amefunga mabao 98 katika mechi 144 akichezea klabu ya Dortmund ligi ya Bundesliga na amesaidia ufungaji wa mabao 172 katika mechi 213 ambazo ameshiriki akichezea klabu hiyo yake ya zamani michuano yote," Arsena wameandika kwenye mtandao wao.

Dortmund ilikuwa imesema kuwa itamuuza mcheza huyo baada ya kupata mbadala wake huku mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi akitarajiwa kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo.
Aubameyang alifunga mabao 141 katika mechi 213 akiichezea Dortmund tangu 2013, ikiwemo mechi 21 kati ya 24 msimu huu.
Lakini alipigwa marufuku na klabu hiyo ya Ujerumani katika mechi yao dhidi ya Wolfsburg tarehe 14 Januari kwa kukosa mkutano wa timu.

Mshambuliaji huyo pia aliwachwa nje kwa mechi yao dhidi ya Hertha Berlin kwa sababu maafisa wa klabu hiyo walihisi hakuwa na malengo lakini alicheza dakika 90 katika mechi ya Jumapili dhidi ya Freiburg.
Ameichezea Gabon mara 56 akifunga magoli 23.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…